Utangulizi wa Mwalimu Kulisha Akili, Kupambana na Njaa

NANI: Waalimu kote duniani watakaopenda kuwatanguliza wanafunzi wao kwa matatizo ya njaa na ukosefu wa lishe wanaweza kutumia makala ya Kulisha Akili, Kupambana na Njaa na miongozo yake kwa masomo.

NINI: Kulisha Akili, Kupambana na Njaa imepangwa kuwa hatua ya mwanzo ya waalimu kuanzisha somo la njaa katika ulimwengu kwa wanafunzi wao. Kwa sababu ya matatizo mbalimbali, tamaduni na mazingira tofauti katika ulimwengu mzima, masomo yamepangwa kama kiunzi cha waalimu huku kukiwa na mazingatio kuwa waalimu watahitaji kurekebisha mipaka yake, lugha, mazungumzo na shughuli zilizotolewa ili kukidhi haja na matarajio ya mazingira ya wanafunzi wao. Viwango vyote vinahusu mada ya ni nini njaa na lishe bora, na ni nani wenye njaa? Ni kwa nini watu wana njaa na kukosa lishe bora na tufanye nini ili tusaidie kumaliza njaa? Kila somo lina malengo yake, dhana, na shughuli zitakazowashughulisha wanafunzi iko katika mijadala kuhusu matatizo haya makubwa na yenye kutokea kila mara.

Masomo matatu yanatolewa kwa viwango vikuu vya elimu vya shule: Cha msingi, kati na upili. Masomo yameelekezwa kati ya maendeleo ya ujuzi ya kila kiwango kinachohusika. Kwa sababu gredi tofauti na umri mbalimbali wa wanafunzi zinafasiriwa kwa njia tofauti kote ulimwenguni, waalimu watahitaji kufanya uchaguzi wa makala zinazofaa viwango vya wanafunzi wao na maendeleo ya bongo zao, huku wakifanya marekebisho yapasayo.

LINI: Siku ya Chakula Duniani, Oktoba 16 na mwaka mzima wanafunzi kote ulimwenguni wanaweza kutumia masomo haya ili kuielewa njaa na ukosefu wa lishe vizuri zaidi. Waalimu wanaweza basi kutoa mawazo yanayotokana na madarasa yao maalum ili waalimu wengine wapate kutumia kote ulimwenguni katika siku zifuatazo za chakula ulimwenguni. Mawazo mapya, shughuli na masomo kutoka kote ulimwenguni yatakusanywa na kusambazwa kila mwaka.

WAPI: Katika darasa lako na katika madarasa mengine maelfu duniani kwa wakati mmoja.

KWA NINI: Mtizamo wetu ni dunia ambapo kila mtu ana chakula cha kutosha ili kuishi maisha yenye afya na yenye kufana bila kuwa na ukosefu wa lishe. Tunaamini elimu na habari kwa masuala yanayohusu njaa ya ulimwengu, kuwepo kwa chakula, na lishe bora kama mambo ya kimsingi kuufanya mwono wa dunia kuwa kweli. Lengo ni kuzua darasa la dunia ambapo watoto na vijana kote watasema na kujadili masuala mamoja, kwa matarajio ya kuwaandaa na kuwasisimua kushiriki katika shughuli ili kujenga ulimwengu usio na njaa.

VIPI: : Unahimizwa kunakili na kutumia makala haya wakati mzima katika mwaka shuleni, huku ukichukua masomo na kuyaelekeza katika mahitaji na hali maalum ya wanafunzi wako na vifaa vya darasani. Masomo yanayochukuliwa na kuendelezwa katika eneo husika fulani yanayohusu jamii mahsusi ndiyo yenye kufaa zaidi. Masomo ya vielelezo yamepangwa kufundishwa dakika 45 kwa kila mojawapo, hata hivyo yanaweza kufundishwa kwa kina kabisa au kijuujuu, upendavyo, kukidhi haja za darasa lako. Habari za kimsingi zinatolewa kwa kila somo na dhana za kutumia ama na wewe mwenyewe na wanafunzi wako, kutegemea utakavyo. Kila somo lina shughuli zinazopendekezwa na hoja za mjadala ambazo unaweza kuzitumia zilivyowasilishwa au unaweza kuzirekebisha ukizitumia kama msingi na mwongozo ili kuzua shughuli zako kwa kila mada.

Kama walimu kote duniani ni vizuri kuamua kifaacho katika tamaduni mbalimbali na mazingira tofauti na kuanza kuyatumia masomo haya ipasavyo, kuanzishwa mfululizo wa vifaa vifaavyo vya kufundishia masuala ya njaa. Tungependa kupokea maoni yenu kuhusu masomo haya na hasa tungependa wewe ushiriki na wengine katika marekebisho uliyofanya. Hali hii itatusaidia sisi kurekebisha programu hii mwaka hata mwaka. Vile vile unahimizwa kuwasilisha masomo au matokeo kutoka madarasa yako yanayoweza kutumiwa na wengine kote ulimwenguni kuhusu mradi huu wakati wa Siku ya Chakula Duniani mwaka ujao (huwa tarehe 16 Oktoba).

Logo

Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora Duniani

Siku ya Chakula Duniani

Washiriki katika

Shukrani

Kudhamini

Wasiliana nasi

Pata faili la mtindo wa PDF