Kuhusu Siku ya Chakula DunianiSiku ya Chakula Duniani husherekewa kila tarehe 16 Oktoba ili kuadimisha kuanzisha kwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), 1945. Nia ya Siku hiyo ni kutoa changamoto kwa umma juu ya maisha ya wenye njaa na ukosefu wa lishe bora, kwa kuwahiza watu ulimwenguni kote kuchukua hatua dhidi ya njaa. Mataifa zaidi ya 150 duniani huadimisha siku hii kila mwaka. Katika Umoja wa Mataifa zaidi ya mataifa 450, yakiwa ya kibinafsi, mashirika ya kujitolea yaliyodhaminiwa na Siku ya Chakula Duniani pamoja makundi ya kienyeji huwa changamoto kwa karibu ya kila jamii. Kwa mara ya kwanza siku hii ilifanyika mwaka 1981, na tangu hapo Siku ya Chakula Duniani imekuwa na mada pekee inayolenga maudhui maalum. 2003 - "Working Together for an International
Alliance Against Hunger" Changamoto inayohusiana ni kampeni ya Chakula-Habari, ambayo inahusisha matangazo ya televisheni, radio, sarakasi na matendo mbalimbali ili kutoa ujumbe mahsusi ya kuwa wakati umefika wa kufanya vitendo kuhusu janga la njaa duniani. Lengo la Chakula-Habari ni kutoa msisimko wa kushirikisha rasilimali ndogo ndogo kwa ajili ya miradi midogo itakayowapa uhakika wa chakula. Michango inayotolewa kwa ajili ya Chakula-Habari, husaidia mamia ya miradi midogo midogo katika nchi zinazoendelea ili kuwasaidia wakulima wadogo kupanda chakula kingi au kwa kuongeza mapato kwa ajili ya kununulia chakula cha kutosha kuwalisha familia yao. Makala ya maudhui ya Siku ya Chakula Duniani/Chakula-Habari ya karibuni yanapatikana katika mtandao wa FAO. |
Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora DunianiUtangulizi wa MwalimuWashiriki katikaShukraniKudhaminiWasiliana nasiPata faili la mtindo wa PDF |