Somo 1: Njaa ni Nini na Wenye Njaa ni Nani?

Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.

Taarifa kwa waalimu

Kwa kuanza kusoma kuhusu njaa duniani ni muhimu watoto kuelewa kazi muhimu ya chakula na umuhimu wa chakula kwa afya bora, ukuaji na kukomaa. Ni muhimu wajue kuwa mataifa na maeneo yote yana watu ambao wana njaa, baadhi yana njaa zaidi kuliko mengine, na kwamba tunashirikiana kutatua tatizo la njaa ulimwenguni. Swala la njaa linafaa kuwasilishwa kwa namna ambayo linahimiza tumaini la mustakabali bora ambapo sote tuna chakula tunachohitaji kwa maisha biabia na yenye afya.

Lengo 1 linatoa jumla ya umuhimu wa chakula tunachokihitaji. Lishe inaelezwa kwa usahihi kama utoaji nguvu na virutubishi kudumisha afya na maisha na kutusaidia kustawi na kukua, bila kueleza kwa kina kuhusu virutubishi mahususi, ambavyo vinaweza kuwa vigumu sana kwa watoto wadogo kuelewa. Masomo ya ziada kuhusu virutubishi, mahitaji mahususi na miongozo ya vyakula vya eneo maalum vinaweza kuongezwa kwa watoto wakubwa kidogo. Kwa uangazaji wa kina wa dhana za virutubishi vya kimsingi, walimu wanaweza kurejelea somo 1 la viwango vyakati na vya upili.

Lengo 2 linatanguliza umuhimu wa kupata aina nyingi za vyakula kukidhi mahitaji yetu ya lishe. Picha sahili inatolewa kuonyesha aina mbalimbali za vykula tunavyohitaji na kuonyesha utaratibu wa kawaida wa lishe unaofuatwa katika sehemu nyingi za dunia na kutoa uanuwai. Muda, kila sehemu inaweza kuwasilishwa kwa kina zaidi na vijitabu na picha kutolewa kwa watoto ili kuzipamba kwa rangi na kujadili.

Lengo 3 linawasilisha kiwango cha tatizo la njaa duniani wa kuwatambua watu walio katika hatari kubwa zaidi ya njaa. Kwa maelezo yenye kina cha jumla kijumla kuhusu hali ya dunia ya sasa, walimu wanaweza kurejea "Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora Duniani" kwenye Utangulizi.

Lengo:

1. Kuelewa kwa nini tunahitaji chakula
2. Kujua kuwa tunahitaji aina nyingi tofauti ya vyakula
3. Kujua ni nani mwenye njaa ulimwenguni