Picha: Tunahitaji Aina Nyingi Tofauti ya Vyakula

Hata kama tutapata chakula cha kutosha kukidhi mahitaji yetu ya nguvu, tunaweza kukosa afya iwapo hatutapata aina tofauti za vyakula tunavyohitaji. Kwa kuwa virutubishi tofauti hupatikana katika vyakula mbalimblai, tunahitaji kula aina nyingi za vyakula ili kupata vitu vyote tunavyohitaji.
Maeneo mengi yana mfumo wa kula vyakula ambavyo vina wingi wa aina mbalimbali vinavyohitajika kwa afya na ukuaji. Kwa mfano, chakula cha msingi kama vile mchele, ngano, mahindi, mihogo au viazi huchukua jukumu la chakula kikuu ambacho huambatanishwa na aina tofauti za mboga, nyama, samaki au kuku, na michuzi kwa kawaida huongezwa. Wakati vyakula vilivyoambatishwa huwa na uanuwai wa mboga, nyama au vyakula vya jamii ya kunde (maharagwe, dengu na njugu), pamoja na michuzi shahamu, sukari na matunda mlo wa asili huwa na utajiri wa virutubishi kwa afya na ukuaji.
| Lengo 3. Kujua ni nani mwenye njaa ulimwenguni |