Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.
Taarifa kwa waalimu
Somo 1 lilitoa habari sahili kuhusu umuhimu wa chakula kwa maisha na afya na kueleza kuwa njaa ipo katika sehemu nyingi za dunia. Katika Somo 2, wanafunzi wanaweza kuangalia mifumo ya chakula kama swala katika njaa ya dunia. Kisha wanafunzi watafahamishwa dhana ya uthabiti wa chakula, kwa kutumia mfano wa nguzo tatu za uhakika wa chakula.
Lengo 1 linawasaidia wanafunzi kuelewa kuwa njaa ipo, kwa kiasi, kwa sababu utaratibu wa kupata chakula ni tata na mfumo huu unaweza kuporomokea (sehemu) yeyote. Kabla ya kutatua tatizo la njaa, sharti tuelewe chanzo cha chakula, na taratibu ambazo baadhi ya vyakula hupitia kabla ya sisi kuvila. Mfumo wa chakula unawasilishwa kwa kutumia hadithi ili kueleza dhana za kimsingi, kwa kuhusianisha maswali ya kujadili.
Lengo 2 linaweka msingi wake katika, kutambulisha dhana za uhakika wa chakula - kuwa na njia ya kupata chakula tunachohitaji ili kuishi maisha biabia na yenye afya - na upatikanaji, ufikaji nguzo zake tatu: na utumiaji wa chakula. Unasisitishwa kuwa mfumo wa chakula sharti usaidie kuwepo na uhakika wa chakula.
![]() | 1. Kuelewa mfumo wa chakula unaowalisha watu |
![]() | 2. Kuelewa maana ya kuwa na uthabiti wa chakula. |