Somo 3: Tunaweza Kufanya Nini ili Kusaidia Kumaliza Njaa?

Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.

Taarifa kwa waalimu

Katika somo lililopita tulisoma kuwa mifumo ya vyakula vya kitaifa na kimataifa ni tata na kila eneo lina matatizo ya kuhakisha kuwa kuna chakuka kwa kila mtu. Somo hili linatupa msingi wa kuelewa yale tunayoweza kufanya binafsi na kwa pamoja ili kupunguza njaa duniani.

Lengo 1 hutumia wazo la kweli au mashujaa wa jadi kuonyesha jinsi watu wanaweza kufanya kazi bila woga kufanya dunia kuwa mahali bora zaidi kwa kila mmoja wetu na huhimiza watoto kufikiria juu ya mashujaa wa kwao ambao wameleta mabadiliko katika jamii zao na pia duniani. Wazo la kimsingi katika mawasilisho yanayotolewa ni kuwa sote tuna mchango katika juhudi za kumaliza njaa na kila mmoja wetu, hata kwa njia ndogo, inaweza kuwa shujaa kwa mtu mwingine.

Lengo 2 linapendekeza hatua mahususi zinzazoweza kuchukuliwa na watoto ili kusaidia kupambana na njaa kwa minajili yao wenyewe, familia zao na jamii zao. Kufanya utafiti maalum kwa maeneo fulani kama msingi wa kuzua mawazo, wanafunzi wanahimizwa kutumia yale waliyojifunza kwa kuboresha jamii zao.

Lengo:

1. Kujua kuwa sote tunaweza na lazima tufanye jambo fulani ili kupambana na njaa
2. Kutambua jinsi ambavyo tunaweza kupambana na njaa katika jamii zetu