Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora Duniani

Ili kuwa na afya na mchangamvu, inatupasa kuwa na chakula cha kutosha, bora na sampuli tofauti ili kutosheleza mahitaji ya nguvu na yale ya madini. Watoto hawawezi kujijenga kikamilifu bila lishe bora na hata watu wazima watapata matatizo katika kudumisha uwezo wao.

Siyo kila mmoja anaweza kupata chakula anachokihitaji na hali hii imesababisha njaa kwa kiasi kikubwa pamoja na ukosefu wa lishe bora duniani. Takribani watu milioni 800 wana utapiamlo mbaya na hawawezi kupata chakula cha kutosha cha kuwapa nguvu za kimsingi. Takribani watoto milioni 200 walio na umri wa chini ya miaka mitano huwa na madhara na ishara za ukosefu wa lishe bora wanapokuwa na ukosefu wa chakula kwa kipindi fulani na wakati wa njaa, na wakati wa mizozo ya kijamii idadi hii huongezeka. Kwa mujibu wa makadirio fulani ukosefu wa lishe bora ni sababu kuu inayosababisha vifo vya takriban watoto milioni 13 walio chini ya umri wa miaka mitano wanaokufa kwa sababu ya magonjwa ya kawaida yanayoweza kuzuilika kama ukambi, kuhara, malaria numonia, au mchanganyiko wa haya magonjwa.

Sehemu kubwa ya watu wenye utapiamlo huishi katika Asia na Pasifiki. Hili ni eneo ambalo lina asilimia sabini ya jumla ya watu katika mataifa yanayoendelea na ina theluthi mbili (Milioni 526) ya watu wenye utapia mlo. Katika nchi ya India pekee kuna watu milioni 204 wenye utapiamlo na eneo la kusini la Asia lina zaidi ya thuluthi moja (milioni 284) ya jumla ya watu wa aina hiyo duniani. Aasilimia nyingine 30 ya watu (milioni 240) huishi Kusini Mashariki mwa Asia na Asia Mashariki ambapo zaidi ya watu milioni 164 ya watu bilioni 1.2 wa China wana utapiamlo. Takriban robo moja ya watu wenye utapiamlo huishi katika Afrika chini ya jangwa la sahara ambalo ndilo eneo lenye kiwango kikubwa cha watu wenye utapiamlo. Hali hii ni mbaya sana katika sehemu ya Afrika ya Kati Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo kuna asilimia 44 wa jumla ya watu wana utapiamlo.

Ukosefu wa lishe bora ndiyo sababu kubwa ya kimsingi ya uzani wa chini wa watoto wakati wa kuzaliwa na ukuaji mbaya. Watoto wenye uzani wa chini wanapozaliwa huwa na matatizo ya ukuaji na magonjwa katika kipindi chao cha utoto, ujana, hadi katika uzima na wanawake waliokuwa na matatizo ya ukuaji huenda wakaendeleza hali hii ya ukosefu wa lishe bora kwa kuzaa watoto wenye uzani wa chini. Uhusiano baina ya ukosefu wa lishe wakati wa ujana – pamoja na kipindi cha kukua mtoto tumboni – na maendeleo ya baadaye maishani, afya mbaya na magonjwa kama ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa sukari, na presha ya damu unaanza kuzuka. Watoto milioni 30 wanazaliwa kila mwaka na matatizo ya kiafya yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora tumboni.

Ukosefu wa lishe bora unaotokana na vitamini muhimu madini muhimu unaendelea kusababisha maradhi mabaya au hata vifo miongoni mwa mamilioni ya watu kote ulimwenguni. Zaidi ya watu bilioni 3.5 wameathiriwa na ukosefu wa madini ya ayani na bilioni 2 wamo katika hatari ya ukosefu wa madini ya ayodini na milioni 200 ya watoto wasiokwenda shuleni wameathiriwa na ukosefu wa vitamini A. Ukosefu wa Ayani unaweza kusababisha matatizo ya ukuaji, upambanaji dhaifu dhidi ya magonjwa na matatizo ya muda mrefu ya maendeleo ya shaksiya na matatizo katika utendakazi wa uzazi, inachangia takriban asilimia 20 ya vifo vinavyohusiana na uleaji wa mimba. Ukosefu wa ayodini unaweza kusababisha uharibifu wa ubongo kabisa, matatizo ya ukuaji, matatizo ya uzaaji, kupunguza kupona kwa watoto tezi. Mama mja mzito anapokuwa katika hali ya ukosefu wa ayodini hali hii inaweza kusababisha hali mbalimbali za matatizo ya ukuaji kwa mtoto wake. Vitamini A inapokosekana hali hii husababisha upofu au vifo miongoni mwa watoto, inachangia vile vile ucheleweshwaji katika ukuaji wa mwili na kusababisha kuzorota kwa uwezo wa mwili kupigana na magonjwa, na matokeo yake ni kuongezeka kwa vifo miongoni mwa watoto wachanga.

Hata kiasi kidogo cha dosari hizi huweza kuzuia maendeleo ya mtoto na uwezo wa kusoma wakati wa ujana wake, na kusababisha kufanya vibaya shuleni, na matokeo yake ni watoto wengi kuondoka shuleni na kuwa na mzigo wa watu wasiosoma. Matokeo mabaya zaidi ya kiafya ya hali hizi tatu ya ukosefu wa lishe bora yanaweza kupunguza kuwepo kwa chakula cha kutosha na vyakula vya aina mbalimbali yanayotoa vitamini muhimu pamoja na madini.

Katika nchi nyingi, matatizo ya kiafya yanayohusiana na wingi wa vyakula bora ni tisho linaloongezeka. Kunona kupita kiasi wakati wa uchanga na ujana ni hali inayohusishwa na matatizo mbalimbali ya kiafya na kuendelea kwake hadi cukubwani husababisha madhara ya kiafya tangu kuongezeka kwa uwezekano wa vifo vya mapema hadi hali za kudhoofisha na ambao huathiri kizazi. Matatizo haya yanayozuka siyo ya nchi zilizoendelea tu bali kuna nchi zinazoendelea zinazokabiliwa na matatizo haya mawili ya utapiamlo na upungufu wa vyakula na magonjwa yanayohusiana na vyakula vilivyozidi. Pia vyuma vizito na dawa za kunyunyizia wadudu ni kizuizi kikubwa cha uboreshaji wa lishe bora katika kila nchi duniani. Matatizo yanayoletwa kupitia vyakula ni mengi katika mataifa mbalimbali, na watoto ndio wahasiriwa wa mara kwa mara- watoto wanapoharisha na kusababisha upungufu wa uzani na kiwango kikubwa cha vifo vya watoto wachanga.

Hata kama ni kwa kiwango kidogo au katika hali zake mbaya sana matokeo ya utapiamlo na afya husababisha hali mbaya katika viwango vya maisha na maendeleo mabaya ya uwezo na kibinadamu. Ukosefu wa lishe bora huweza kusababisha hasara katika kuzalisha mali na hasara za kiuchumi kwa kuwa watu wazima walioathiriwa na hali ya ukosefu ya lishe bora na athari nyingine hawawezi kufanya kazi kikamilifu; hasara za kielimu, kwa kuwa watoto hudhoofishwa au kuugua kiasi cha kutoweza kwenda shuleni au kusoma vizuri, gharama za kiafaya maana inabidi kunguza watu wanaougua maradhi yanayosababishwa na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora; na vile vile gharama za kuangalia na kutunza walemavu na wakati mwingine familia zao.

Katika karne iliyopita, kulikuwa na juhudi kubwa katika kuongeza siyo idadi ya chakula tu bali ubora wake na kuongeza hali ya kiafya ya watu. Huku utoaji wa vyakula duniani ukienda sambamba na ongezeko la idadi ya watu, na afya, elimu na huduma za kijamii zimeboreka kote duniani kwani idadi ya wenye njaa na wanaokosa lishe bora imepungua kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo kupata vyakula mbalimbali vya kutosha na visivyo na madhara bado ni tatizo kubwa katika nchi mbalimbali, hata pale pasipo na chakula cha kutosha katika kiwango cha taifa. Katika kila nchi aina moja au nyingine ya ukosefu wa lishe na njaa huendelea kuwepo kwa mfumo tofauti.

Kumaliza njaa huanza tu pale ambapo kuna chakula cha kutosha kinachozalishwa na cha kutosha kwa kila mtu. Hata hivyo, kupanda chakula cha kutosha hakumaanishi njaa yaweza kumalizwa. Uwezekano wa watu wote nyakati zote kupata chakula bora cha kutosha na kisicho na madhara kwa maisha yenye afya - usalama wa chakula lazima uwepo. Ongezeko la juhudi almradi kuhakikisha kuwepo kwa chakula zinahitajika ili kumaliza njaa na hali ya ukosefu wa lishe bora na athari zake mbaya miongoni mwa vizazi vya sasa na vijavyo; kote duniani. Mchango wa kila mmoja wetu kupitia kubadilishana kwa habari, kujali na kushiriki katika shughuli - ni muhimu katika kuhakikisha ni haki ya kila binadamu kuwa huru kutokana na njaa.

Tarama pia karatasi ya Siku ya Chakula Duniani na masuala Mbalimbali "Kikwi kisicho na Njaa" Hupatikana katika hali iliyochapwa na pia kwenye Mtandao www.fao.org