Somo 1: Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora ni nini? Na ni Nani aliye na Njaa?

Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45-60, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.

Taarifa kwa waalimu

Ili kuanza somo lao kuhusu njaa ya dunia, ni muhimu wanafunzi kuelewa kazi ya chakula kwa afya bora, ukuaji na maendeleo. Wanapaswa kujua kuwa nchi zote na maeneo yote wana watu walio na njaa, maeneo wengine zaidi kuliko mengine, na tunafanya kazi pamoja ili kusuluhisha tatizo la njaa. Mada ya njaa inafaa kuwasilishwa kwa njia itakayoweka matumaini kwa siku za usoni ambapo sote tutakuwa na chakula cha kutosha kwa maisha bora.

Lengo 1 linatoa jumlisho ya umuhimu wa kupata virutubishi tuvitakavyo. Lishe bora inawasilishwa kama kitu kinachotoa nguvu na virutubishi ili kudumisha afya na maisha na kutusaidia kukua. Ikiwa ni somo la juu la vitamini na madini linafaa, maelezo yake kwa urefu yatapatikana katika Somo 1 ya kiwango cha Upili.

Lengo 2 hutanguliza umuhimu wa kupata sampuli za vyakula ili kutosheleza mahitaji yetu ya lishe bora. Picha rahisi inawasilishwa ili kuonyesha aina mbalimbali za vyakula tunazohitaji na kuonyesha ruwaza ya ulaji inayofuatwa katika nchi nyingi ulimwenguni na inatoa sampuli za vyakula.

Lengo 3 linatoa mipaka ya tatizo la njaa na kutambua wale ambao wamo katika hatari ya kuathiriwa. Ni muhimu kwa wanafunzi kuelewa uzito wa tatizo, bila kuonekana huwezi kufanya lolote lile. Njia moja ya kufanya hivi ni kusisitiza kuwa nchi zote na maeneo yote yana njaa kwa kiwango fulani na tunafanya kazi pamoja kutatua hili tatizo. Habari zaidi zinazotoa durusu ya hali ya dunia, zinapatikana katika utangulizi wa "Njaa na Ukosefu wa Lishe bora Duniani"

Lengo:

1. Kuelewa matokeo ya njaa na ukosefu wa lishe bora
2. Kujua kuwa tunahitaji aina tofauti ya vyakula
3. Kujua ni nani aliye na njaa na aliyekosa lishe bora duniani