Dhana:Chakula cha kutosha ni muhimu kwa maisha biabia na yenye afya
Yaliyomo
Chakula ni muhimu kwa maisha. Ili kuwa na afya bora lazima tuwe na chakula katika viwango vya kutosha, bora na sampuli tofauti za vyakula na chakula kiwe salama. Watoto na vijana hawawezi kujenga uwezo wao bila lishe bora na watu wakubwa watakuwa na shida katika kupanua na kudumisha uwezo wao.
Chakula hutupa nguvu tunazohitaji kukua na kutekeleza shughuli za kimwili na kazi za kimsingi za mwili (kupumua, kuwaza, kudhibiti joto la mwili, mwendo wa damu na umeng'enyaji chakula. Hutusaidia vile vile na viambajengo vya kujenga na kudumisha mwili na kutoa kinga kwa magonjwa.
Kazi hizi mbalimbali huwezeshwa tu na virutubishi vilivyomo katika chakula kabohidrati, protini, shahamu, vitamini madini na maji. Vyakula vyote hivi vina virutubishi kwa viwango tofauti. Kila aina ya virutubishi hufanya kazi fulani. Hii ndiyo sababu ni vizuri na kuwa sampuli nyingi za vyakula katika ulaji wetu maana ni muhimu kwa afya bora. Tunahitaji virutubishi vyote vinavyotokana na vyakula mbalimbali kwa mifanyiko yote ya miili yetu.
Chakula kingi zaidi au kutokuweko na chakula cha kutosheleza huweza kusababisha afya mbaya na humfanya mtu kupata magonjwa kama kunenepa kupita kiasi, magonjwa ya mishipa ya moyo na ugonjwa wa sukari.
Lishe bora pia hutegemea jinsi chakula kinavyowekwa kwa hali ya usalama ili kiweza kulika na pia kuhifadhi hali yake ya urutubishaji.
Matendo
Jadili mambo yaliyo hapo juu na hoja zipangwe kulingana na wakati na kulingana na msingi wa wanafunzi pamoja na matakwa yao. Waeleze wanafunzi kuwa chakula kina vitu vilivyo muhimu kwa maisha. Baadhi ya arki hizi ni kidogo sana kiasi kwamba hatuwezi kuziona, lakini bila kuwa nazo miili yetu haiwezi kufanya kazi vilivyo. Vitu hivi hupatikana katika vyakula Lakini katika aina mbalimbali za vyakula, kwa hiyo lazima tule vyakula vya sampuli mbalimbali ili kuhakikisha kuwa tunapata arki hizi katika ulaji wetu.
Karatasi ya ukweli ya Chakula Hutupa inatoa habari za jumla kuhusu lishe bora, pamoja na kazi za virutubishi vya nguvu. Protini, wanga mafuta. Vyanzo vya vyakula vimepangwa kwa virutubishi vitatu hivi vya nguvu, pamoja na vitamini na madini: vitamini A, vitamini B, vitamini C, vitamini D na ayodini. Toa au onyesha karatasi ya ukweli mjadiliane virutubishi vilivyopangwa. Waulize wanafunzi waandike orodha ya vyakula wanavyovila katika siku za kawaida, ili uone kama vyakula vyao ni vya sampuli mbalimbali na viwezavyo kutoa virutubishi vilivyoorodheshwa. Kwa mfano, vyakula vyao vina protini, vitamini A au chuma? Ikiwa orodha yao haina vyakula hivyo vilivyo na virutubishi vilivyooroodheshwa, jadiliana nao kuhusiana na vyakula ambavyo vingeongezwa kwa ulaji wao ili kuwapa virutubishi vinavyohitajika.
Dhana: Njaa huathiri usalama wa watu, mataifa na dunia
Yaliyomo:
Nguvu za taifa lolote hutegemea nguvu za watu wake. Watu wakiwa na afya bora nguvu na siha nzuri, wana nguvu, ubunifu, usalama na ushupavu wa kutatua matatizo, kubuni kazi kuu za kisanaa na muziki, kuchangia maendeleo ya kisanyansi na kuishi maisha yao ya kawaida kwa furaha na heshima, hatimaye kujenga utamaduni wao kwa viwango vikuu. Wananchi wanaolishwa vyema ni wananchi walio na uwezo wa kutoa huduma na ndio wanaochangia jamii yao. Watu wasio na siha nzuri hawana nguvu za kufanya kazi au kusoma na kila mara huhitaji huduma za kiafya. Gharama kwa uwezo uliopotea pamoja na mfumo wa kiafya huweza kukwamisha jamii.
Matendo
Jadili masuala yaliyoorodheshwa hapo juu pamoja wanafunzi. Waulize waorodheshe watu maarufu katika jamii yao, nchi yao au dunia kuanzia wakati uliopita au wakati wa sasa. Orodhesha majina ya watu wengine, ambao wanafunzi wangeweza kuwataja ambao wameathiri hali ya mambo duniani. Waulize wanafunzi wafikirie tofauti ya ulimwengu ulimwenguni kama watu hawa wangekuwa na ukosefu wa lishe bora, wangekuwa na njaa au wagonjwa kiasi wasingeweza kufanya kazi walizofanya. Waambie wanafunzi umuhimu wa kila mmoja wetu duniani kutenda kazi kwa uwezo wote tulio nao. Karama zilizopotezwa zinatuathiri sisi wote.