Lengo 2: Kujua kuwa tunahitaji aina tofauti ya vyakula

Vifaa:
Picha: Tunahitaji Aina Nyingi Tofaut...ya Vyakula
Dhana : Watu wanahitaji vyakula vya aina mbalimbali ili kuwa na afya bora na kukua vyema
Yaliyomo
- Hata kama tutapata chakula cha kutosha kutosheleza mahitaji yetu ya nguvu, tunaweza kuwa bado na afya mbaya ikiwa hatuwezi kupata sampuli za kisawasawa za vyakula mbalimbali tunavyovihitaji. Kwa sababu virutubishi tofauti vinapatikana katika vyakula tofauti, inatupasa kula vyakula vya aina mbalimbali ili kupata vitu vyote tunavyovihitaji.
- Maeneo mengi yana mpangilio wa kijadi wa kula na kupata sampuli mbalimbali zinazohitajika kwa ukuaji. Kwa mfano, chakula cha msingi kama mchele, ngano, mahindi, mhogo, au viazi vitakuwa vyakula vya kimsingi, na kuandamana na vyakula vingine vidogo kama mboga, nyama, samaki au kuku na michuzi. Wakati ambapo vyakula vya mwanadamu huwa na mboga za sampuli mbalimbali, nyama au nafaka (maharage, kunde na njugu) pamoja na michuzi iliyo na mafuta na sukari, ulaji wa kijadi utakuwa na virutubishi vinavyohitajika kwa afya na ukuaji.
Matendo
- Waeleze wanafunzi kuwa watu kote ulimwenguni wana njia tofauti za ulaji. Sambaza au onyesha picha ya Tunahitaji Aina Nyingi Tofauti ya Vyakula na ueleze kuwa chakula kinachoandiliwa familia hii kinajumlisha sehemu kubwa ya chakula cha msingi kama maboga ya stachi au nafaka. Waulize wanafunzi kinaonekana vipi (mchele, mhogo, na viazi) Waulize wanafunzi ni kipi kingine wanachokiona katika viwango vidogo (matunda, nyama, vipande vya mboga na michuzi).
- Waeleze wanafunzi hivi ndivyo watu wengi duniani hula. Wana chakula cha msingi, kisha wanaongeza viwango vidogo vya vyakula vinavyoandamana nacho. Jadili ni kwa vipi vyakula vya msingi kote duniani kwa kawaida huwa ni vya stachi kama mchele, na nafaka nyingine, viazi na mhogo. Jadili ni kwa vipi vyakula vya kuandamana huenda vikawa mboga maharagwe, kunde, njugu, nyama, samaki, yai au michuzi iliyotengenezwa kutokana na vyakula hivi.
- Waeleze wanafunzi kuwa vyakula vya kuandamana hutoa aina tofauti za virutubishi tunavyo hitaji ili kuwa na afya bora. Na kwamba tujaribu kula hivyo vyakula tofauti kila siku. Tujaribu kula matunda baada ya chakula au badala ya vyakula viepesi.
- Waulize wanafunzi aina zao za vyakula na uwaulize kama wana vyakula vya msingi vinavyoliwa na vyakula vya kuandamana kama familia iliyo katika picha.
- Ukitumia picha kama mwongozo uliza wanafunzi kubuni orodha ya vyakula vyao vya kienyeji vya msingi na vyakula vya kuandamana navyo. Shughuli hii inaweza kuunganishwa na ile ya awali kwa kutumia orodha ya vyakula vya awali, ikiwa vinafaa. Uliza wanafunzi kuhesabu ni vyakula vingapi vya kuandamana wanavyoweza kuorodhesha na kueleza ni kwa vipi kuwepo kwa vyakula vingi kunatoa virutubisho wanavyohitaji kukua na kuwa na afya bora.
