Lengo 3: Kujua ni nani aliye na njaa na aliyekosa lishe bora duniani
Vifaa
Picha: Ramani ya Njaa Duniani
Karatasi ya Ukweli: Nani aliye Hatarini?
Dhana:
- Njaa ni kutopata chakula cha kutosha au aina za vyakula vya kutimizia mahitaji ya lishe
- Kila nchi na maeneo yana baadhi ya watu wenye njaa
Yaliyomo
- Hali ya njaa ni kutokuwepo na chakula cha kutosha na kutokuwepo na sampuli za vyakula vinavyohitajika ili kutosheleza mahitaji ya lishe bora. Njaa ni tatizo la dunia nzima. Kila nchi na kila eneo lina watu fulani wasiopata chakula cha kutosha. Hata kama njaa ipo katika kila nchi, nchi fulani zina matatizo makubwa zaidi ya kulisha watu wake.
- Katika mwaka 2001, watu milioni 800 wana njaa na hawana cho chote cha kula katika kipindi cha mwaka mzima. Lengo la kikwi mpya ni kuhakikisha kila mtu ana chakula cha kutosha na katika sampuli zifaazo.
- Njaa inasababishwa na sababu mbalimbali na itahitaji juhudi kubwa kutatua matatizo yanayosababisha njaa. Watu wengi wanafanya kazi katika sehemu mbalimbali za dunia ili kutambua na kutafuta suluhu kwa tatizo la njaa.
- Watu wote, wakiwemo wanafunzi, wanaweza kuwa sehemu ya juhudi hili dhidi ya njaa kwa kusoma habari za njaa na kusoma jinsi ya kuizuia.
Matendo
- Onyesha Ramani ya Njaa Duniani inayoonyesha maeneo yenye matatizo makubwa ya njaa na ukosefu wa lishe bora. Eleza jinsi ramani inaonyesha maeneo ambapo watu wengi hawapti chakula chote wakitakacho. Onyesha maeneo yenye watu wengi wenye matatizo ya njaa. Eleza kuwa kila nchi ina watu wenye njaa.
- Tambua eneo lako la dunia na ujadili tatizo la Njaa la eneo lako. Uliza wanafunzi waeleze ikiwa wanajua anayeweza kuwa na njaa katika eneo lao.
- Jadili jinsi njaa inavyotokea kwa sababu mbalimbali, na jinsi inavyohitaji kazi kubwa na juhudi kutatua tatizo hilo, na jinsi watu wengi wanavyofanya juhudi kusoma kwa nini watu wana njaa na kutafuta njia kuhakikisha kwamba kuna chakula kizuri, katika kipindi cha mwaka, kwa kila mtu.
- Jadili kuwa watu walio duniani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kila mtu awe na chakula cha kutosha na sampuli zifaazo za vyakula.
Dhana:Njaa na ukosefu wa lishe bora upo kwa namna fulani katika kila nchi duniani, miongoni mwa vikundi vilivyo hatarini kuathirika
- Ingawa baadhi ya nchi zina watu wengi zaidi wenye njaa - kwa idadi na asilimia ya watu wake - hakuna nchi ulimwenguni isiyo na njaa na ukosefu wa lishe bora. Ili kuweza kufanya jitahada mahususi za kutatua tatitzo la njaa, lazima kwanza tujue nani wenye njaa.
- Karatasi ya ukweli Nani Aliye Hatarini? Inatupa orodha ya vikundi vilivyo kwenye hatari ya kuathiriwa ulimwenguni kote. Jadili jinsi, katika kila eneo watu walio hatarini kupata njaa, ni masikini, watu wasio na elimu au uhakika wa kazi, watu wasio na ardhi ya kulima mazao ya chakula na watu wanahitaji virutubisho fulani muhimu mwilini, kama watoto (ambao huhitaji kukua) na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha/kulea. Vita, machafuko katika jamii, kubadilika badilika kwa hali ya hewa na mazingira, na matukio mengine ya kushtukiza kama mafuriko, tetemeko la ardhi nayo huchangia kwa pamoja hali ya njaa kwa kipindi kifupi au kirefu.
Matendo
- Rudia orodha ya vikundi viathirika iliyopo kwenye karatasi ya ukweli Nani Aliye Hatarini?. Kama muda unaruhusu, waulize wanafunzi ni kwa nini kila kikundi kina hatari ya kuathiriwa na tatizo la njaa na ukosefu wa lishe bora.
- Husisha matatizo ya njaa katika eneo lako na maeneo mengine yaliyoathiriwa. Ni watu wangapi wenye njaa wanatokana na makundi yaliyoathiriwa na kuorodheshwa? Kwa mfano, je tatizo la njaa katika eneo lako linahusiana na kupata migongano, kwa wale hawakubahatika katika jamii wenyeji au ugenini? Waulize wanafunzi kama wanaweza kufikiria juu ya makundi mengine katika eneo lao yanayoweza kuwa makundi hatarini kuathiriwa na njaa, na kwanini.
Muhtasari
Somo 1 limewatanguliza wnafunzi kwa umuhimu wa chakula kwa ukuaji na kazi za kimwili ili kuwapa muktadha wa kuzungumzia suala la njaa. Mipaka na mtazamo wa kidunia wa njaa yaliwasilishwa, pamoja na durusu ya makundi hasiriwa kote ulimwenguni. Baada ya kumaliza somo la kwanza wanafunzi wanapswa kueleza kuwa:
- Chakula na virutubishi vyake ni muhimu kwa maisha.
- Tunahitaji sampuli za vyakula kwa afya bora.
- Ulaji mwingi wa kijadi ulio bora una vyakula vya msingi vya stachi na vyakula vya kuandamana katika idadi ndogo.
- Nchi zote zina matatizo ya njaa na ukosefu wa lishe bora.
- Makundi fulani yanaathiriwa sana na njaa.
- Njaa inaathiri kila mtu duniani.
Kwa kujiunga na Foramu ya KAKN, bonyeza HAPA.
