Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.
Somo 1 liliwasilisha habari kuhusu umuhimu wa chakula kwa maisha na afya na pia lilieleza kuwa njaa ipo katika sehemu nyingi duniani. Wanafunzi wanafaa kuelewa kuwa njaa na ukosefu wa lishe bora linasababishwa na kuendelezwa na sababu fulani, zote ambayo yanasababisha kushughulikiwa kuhakikisha kuwa wote wanapata chakula wanachokihitaji kwa maisha biabia na maisha yenye afya. Katika Somo 2 wanafunzi wanaweza kushughulikia mifumo ya vyakula kama suala katika njaa ya dunia. Wanafunzi watatangulizwa kwa wazo la kuwepo kwa chakula, kutumia mfano wa nguzo tatu za kuweko kwa chakula.
Lengo 1 linasaidia wanafunzi kuelewa kuwa njaa ipo, kwa sababu utaratibu wa kupata chakula ni ngumu na mfumo unaweza kuharibika mahali popote. Kabla ya kusuluhisha tatizo la njaa lazima tuelewe chakula kinatoka wapi na taratibu ambamo vyakula fulani hupitia kabla ya sisi kuvila. Mfumo wa chakula unawasilishwa kwa kutumia hadithi inayoeleza mawazo ya kimsingi, na maswali ya mjadala yakiwemo.
Lengo 2 linaendeleza mawazo yaliyowasilishwa katika lengo 1 yanayohusu mifumo inayolisha watu na kutanguliza wazo la kuwepo kwa chakula-kuweza kufikia chakula tunachokihitaji wakati wote tunahitaji ili kuishi maisha ya biabia na yenye afya. Inasisitiza haja ya kuhakikisha watu wote wana siha nzuri na wana chakula cha kutosha. Nguzo tatu za kuwepo kwa chakula - upatikanaji, ufikiaji na matumizi ya chakula - yanatangulizwa ili kutoa msingi wa matendo dhidi ya tishio la utoaji wa chakula.
![]() | 1. Kuelewa mfumo wa chakula unaolisha watu |
![]() | 2. Kuelewa maana ya kujitosheleza kwa chakula |