Lengo 1:
Kuelewa mfumo wa chakula unaolisha watu
Vifaa
Hadithi: Hadithi ya Nyanya za Miguel
Picha: Hatua katika Mfumo wa Chakula
Jedwali: Jedwali ya Mfumo wa Chakula
Dhana:Mfumo unaotoa chakula una hatua nyingi
Yaliyomo
Hatua za mfumo wa chakula ni pamoja na:
- Kujitayarisha kwa upanzi
- Kupanda chakula
- Kutoa chakula shambani
- Kuandaa, kuuza au kuhifadhi chakula
- Kuandaa na kula chakula.
Kila ya hatua inajumlisha hatua nyingi na mazingatio. Kila utaratibu huenda Ukahusisha watu wengi, kama vile wafanyikazi wa benki, wachukuzi wa kilimo, wakulima na wafanyikazi wa shambani, madereva wa lori, wanaohusika na chakula, wasagishaji, pia na masharti tofauti, kama vile hali ya hewa, barabara, na hali ya utulivu wa kiuchumi na kisiasa. Ni utata huo unaofanya utoaji wetu wa chakula kuwa na matatizo.
Idadi ya hatua zilizoko na taratibu katika mfumo hutegemea hali fulani maalum kwa kila jamii na familia. Mifumo ya kinyumbani, kikiwemo kilimo cha nyumbani, na mashamba madogo, huenda vikapunguza utata wa taratibu unaohusika, au hata kuondoa kabisa hatua kama uchukuzi, kuandaa na kuuza.
Kufuga wanyama wadogo na kupanda mimea huweza kuongeza uhakika wa familia kwa kutoa chakula cha kutosha kwa familia pamoja na pato kwa kuuza chakula cha ziada.
Hata hivyo hata mashamba ya nyumbani huenda yakategemea
watu wengine kwa kutoa mahitaji kama mbegu, vifaa, mbolea, usagishaji wa nafaka
au kukodisha mashamba na mashine ya shambani. Na mashamba yote, madogo kwa
makubwa yanaweza kuhasiriwa na hali ya hewa. Tazama Jedwali ya mfumo wa
chakula ili uone sababu zilizomo katika kila hatua katika mfumo wa chakula na ulinganishaji wa baadhi ya tofauti kati ya mifumo ya kinyumbani na ya kibiashara.
Hadithi ya Nyanya za Miguel imeandaliwa kuanzisha majadiliano kuhusu kila mojawapo ya hatua katika mfumo wa chakula. Inaweza kusomwa kwa wanafunzi wadogo ili kuonyesha jinsi chakula kinavyopandwa, kusafirishwa na kuandaliwa.
Wanafunzi wakubwa wanaweza kusoma hadithi wenyewe au katika vikundi. Majadiliano yanaweza kufanywa kwa kina kwa wanafunzi wakubwa, waulize tena wafikirie hatua zozote za ziada zinazoandamana na kila hatua katika safari ya nyanya na kitakachofanyika mambo yakiharibika (ukosefu wa mvua, Miguel aliugua na hangeweza kuangalia mimea, lori lililoelekea jijini liliharibika na nyanya ziliharibika, n.k.) Mwalimu anaweza kuongoza majadiliano kuhusu matokeo ya kuharibika kwa mfumo wa chakula kwa utoaji wa chakula kwa jamii.
Ikiwa Hadithi ya Nyanya za Miguel haitoshelezi umri fulani shughuli ya badala imewekwa inayoangalia vyakula vya kienyeji kupitia mfumo wa vyakula.
Matendo
Kujitayarisha kwa upanzi wa chakula:
- Miguel alihitaji nini kwa ajili ya tamata zake? Mbegu, mbolea, jembe la kukokota na shamba. Kitu kingine.
- Kungefanyika nini kama ikiwa hivi vitu visingekuwepo
na Miguel angepata nyanya bila vifaa na vitu hivi?
Upanzi wa chakula:
- Miguel alihitaji nini ili nyanya zipate kukua? Jua, mvua na mikono yake kufanya kazi, kupalilia na kuziangalia nyanya (nguvu zake). Kitu kingine?
- Nyanya za Miguel zingekuwa kama hizi hazingekuwepo?
Kutoa chakula shambani:
- Nyanya za miguel zilipelekwa wapi baada ya yeye na Ana kuzichuma?
- Baadhi zilipelekwa kwa nyumba ya Miguel na ya Ana ili kuliwa kwa chakula cha jioni au kutiwa katika mitungi kwa minajili ya kuzihifadhi.
- Baadhi zilipelekwa kijijini sokoni na Miguel kwa mkokoteni.
- Sokoni kijini ziliwekwa kwenye lori na kupelekwa jijini.
- Baadhi zilipelekwa katika soko la jijini.
- Baadhi zilipelekwa katika kiwanda cha chakula.
- Nyanya zilisafirishwa mwendo gani ili kutumiwa kwa chakula cha jioni cha Miguel na Ana?
- Nyanya zilisafirishwa mwendo gani ili kufika jijini? Safari hii ilifanywa vipi? (Mkokoteni wa Miguel na lori la Pedro.)
- Nyanya zingekuwaje endapo mkokoteni na lori
lingeharibika njiani?
Maandalizi ya uuzaji wa chakula
- Nyanya zimeandaliwaje na Ana?
- Miguel ameziuzaje nyanya zake?
- Pedro akiwa kama kiungo cha kati nyanya ameziuzaje?
- Katika kiwanda cha chakula, kimetokea nini wakati wa matayarisho ya nyanya?
- Ni kwa kwanini hizi hatua ni muhimu katika utoaji wa
chakula? Kingetokea nini kama chakula kisingeandaliwa na kipatikane hapo
baadaye?
Kula chakula:
- Jadili ni kwa vipi watu wanahitaji pesa kununua chakula ikiwa hawatapanda chakula chao kama Miguel na Ana.
- Jadili ni kwa vipi watu lazima waelewe jinsi ya kutumia chakula kwa usalama na kuchagua vyakula vya kuwafanya kuwa na afya bora.
- Jadili matatizo yanayoweza kutokea na kila moja ya hatua hizo na vipi chakula hakingekuwepo kwa minajili ya kuliwa na watu.
- Jadili tofauti baina ya nyanya zilizotumiwa moja kwa
moja na Miguel na Ana kutoka mashambani na nyanya zilizorudi zikiwa kwenye
mkebe.
Kuhifadhi chakula:
-
Wazo muhimu la kuzingatia ni uharibifu wa chakula
unaotokea kwa sababu ya wadudu na uharibifu katika viwango vya masoko na
nyumbani. Kulinda chakula kutokana na wadudu, panya, unyevu, na uharibifu
huweza kuongeza, kwa kiasi kikubwa, chakula ambacho huweza kuwepo kwa matumizi
ya watu. Kila mwaka utaratibu wa baada ya kuvuna huharibu mamilioni ya tani ya
vyakula. Jadili umuhimu wa kulinda chakula kutokana na wadudu na uharibifu na
jinsi Ana na waandaaji wengine wa chakula huzingatia uharibifu wa chakula.
Matendo badala
Ukitumia Jedwali la mfumo wa chakula kama kielelezo andaa jedwali ambapo wanafunzi wataorodhesha taratibu na mazingatio ya kila mojawapo ya hatua zilizo katika mfumo wa chakula wanachotegemea kwa chakula katika jamii yao. Chagua chakula kimoja au zaidi kinacholiwa mara kwa mara huku ukianza mwanzoni kabisa onyesha jinsi mfumo wa chakula unavyofanya kazi. Jadili ambapo mfumo huo wa chakula unaweza kuathiriwa. Ikiwa, kwa mfano, mfumo wa chakula unategemea sana kilimo cha kibiashara, kungefanyika nini ikiwa wafanyikazi wa shambani hawangekuwepo, ikiwa ukame mbaya ungetokea, ikiwa, kwa ghafla, njia zote zinazoelekea jijini zingefungwa, n.k.?
