Lengo 2: Kuelewa maana ya kujitosheleza kwa chakula

Vifaa
Utafiti Maalum wa Nchi
Dhana:
- Kuwa na uthabiti wa chakula inamaanisha kuwa na uwezo wa wakati wote kufikia chakula tunachohitaji kwa maisha biabia na yenye afya
- Nguzo tatu za uhakika wa chakula ni upatikanaji na matumizi ya
chakula
Yaliyomo
- Uthabiti wa kwa chakula unaelezwa kuwa uwezekano wa watu wote, nyakati zote, kupata chakula cha kutosha cha virutubishi vya kutosha na salama (thamani, kiasi, na sampuli) kwa maisha ya biabia na afya nzuri.
- Lazima tuwe na hali ambayo watu wote wanaweza kupata chakula wanachokihitaji na wawe na siha nzuri katika njia ya heshima na ya kudumishwa.
- Kuwepo kwa chakula huathiriwa na mambo mbalimbali yakiwemo kimsingi utoaji wa chakula na kupata kazi na huduma za msingi kama elimu, huduma za afya usafi, maji safi na nyumba zenye usalama.
- Umaskini, ukosefu wa usawa wa kijamii na ukosefu wa elimu ni mambo makuu yanayosababisha njaa na ukosefu wa lishe bora na ni vizingiti vikubwa katika uthabiti wa chakula.
- Uthabiti wa chakula hauwezi kuweko kwa kuzalisha chakula kingi. Ikiwa watu hawawezi kuweza kununua chakula kilichoko, ikiwa ulaji wao hauna vitamini muhimu na madini au ikiwa kuna uharibifu wakati wa kukiandaa na ugawaji kutofanya chakula kisiwe salama kwa ulaji basi hawatakuwa na uthabiti wa chakula.
- Uhakika wa chakula unategemea nguzo tatu, au miguu ya kuhimili.
- Chakula lazima kipatikane, kumaanisha kuwa kiasi cha kutosha chenye ubora na salama lazima kizalishwe au kuagizwa kwa viwango vya taifa na maeneo ya kawaida.
- Chakula lazima kiweze kufikiwa, kumaanisha uhakika lazima kisambazwe na kuweza kupatikana katika eneo husika, na lazima kila mtu aweze kumudu kukinunua.
- Chakula lazima kitumiwe kwa njia nzuri iwezekanavyo ili kila mtu uhakika na afya na siha nzuri (kitoshe kwa wingi, ubora na uanuwai kulingana na mahitaji na kila mtu).
- Ili kupata uthabiti wa kitaifa wa chakula nchi lazima iweze kuzalisha au kuagiza chakula inachokihitaji, na iweze kukihifadhi, kugawa na ihakikishe kunao usawa katika migao yake.
- Ili familia ziweze kuwa na uthabiti wa chakula lazima ziwe na uwezo wa kuzalisha chakula au kuhakikisha mahitaji ya lishe ya familia yote yanatoshelezwa.
- Kuanzia na uelewa wa utata wa mfumo wa chakula, wanafunzi wanaweza kutatua hali maalum zinazokabiliwa na nchi kuona ikiwa masuala ya njaa yanahusiana na kuwepo kwa chakula, ufikiaji au matumizi ya chakula. Uelewaji wa mambo yanayohusika ndiyo hatua ya kwanza ya kutatua tatizo hilo.
- Tunaweza kujifunza mambo muhimu kwa kuangalia mataifa ambayo yameweza kupunguza na kulinganisha hali zao na zile za nchi ambazo zimekuwa na matatizo katika hali ya lishe bora. Kulinganisha hali na kuangalia ruwaza kunaweza kudhihirisha sababu zinazochangia njaa na suluhisho la njaa kote ulimwenguni. Tafiti maalum za nchi zenye matatizo ya njaa zimetolewa.
Matendo
- Jadili ni kwa jinsi gani hali ni tofauti kutoka eneo fulani hadi jingine, na jinsi muungano fulani wa hali husababisha matatizo ya uthabiti wa chakula. Unapochunguza nchi zenye viwango tofauti vya mabadiliko vya hali za uthabiti kwa chakula na kulinganisha hali zilizo katika kila mojawapo ya nchi, mwelekeo unaweza kubainika unaoashiria uthabiti wa chakula katika kila nchi.
- Tafiti maalum za nchi zinatolewa na kuonyesha tofauti kati ya hali zilizopita na hali za sasa katika nchi zilizochaguliwa ambapo mabadiliko katika uthabiti wa chakula na njaa yamekuweko kwa miongo michache iliyopita. Tafiti maalum zinawasilishwa na eneo katika jozi ukilinganisha nchi ambayo imefanikiwa katika mapambano ya njaa na ile ambayo imeshindwa kabisa kulisha watu wake. Wape wanafunzi kusoma mmoja mmjoa au katika vikundi kusoma jozi moja ya utafiti maalum kila mmoja, au jadili shemu iliyochaguliwa darasani. Huku mwalimu akitoa usaidizi, wanafunzi waelezwe kujadili sababu zinazosababisha hali ya sasa ya njaa katika kila nchi. Weleze wanafunzi wajadili hali zinazohusiana na njaa kwa upande wa uwepo, upatikanaji na matumizi ya chakula.
- Anzisha majadiliano ya mfumo wa chakuka jadili jinsi hali kama hiyo ingekuwa katika maeneo yao.
Muhtasari
Lengo tunalo la kuhakikisha watu wote duniani wana chakula cha kutosha. Kupata chakula kunahusisha hatua nyingi. Lazima tuelewe kinakotoka chakula chetu ili kufanya uamuzi jinsi ya kulisha kila mtu.
Somo 2 lilidhihirisha utata wa mfumo wa chakula kueleza sababu nyingi kuwa watu wanaweza kuwa na njaa na kutanguliza wazo la uthabiti wa chakula. Baada ya kumaliza Somo 2, wanafunzi wanapaswa kueleza:
- Uthabiti wa chakula unamaanisha kuweza kufikia chakula tunachokihitaji kwa maisha ya biabia na afya bora nyakati zote.
- Uthabiti wa chakula hutegemea nguzo tatu: chakula lazima kipatikane, kifikike na lazima kitumiwe kwa njia bora ili kila mtu awe na afya na siha nzuri.
- Mfumo unaotupa chakula unahusu hatua nyingi. Utata wa utoaji wa chakula unapoongezeka uwezekano wa kuzuiliwa katika utoaji wa chakula hutarajiiwa.
Tunaweza kufanya kazi pamoja kupunguza njaa. Somo 3 litachunguza kile tuwezacho kufanya kusaidia kupunguza njaa katika dunia yetu.
Kwa kujiunga na Foramu ya KAKN, bonyeza HAPA.
