Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.
Wanafunzi inafaa waelewe njaa popote pale ulimwenguni huathiri kila mtu; mahali pote tunakohusika kuhusiana na suala la njaa na ukosefu wa lishe bora na kwamba kuna hatua maalum zinazoweza kuchukuliwa na kila mmoja wetu sisi kupata dunia isiyo na tatizo la njaa. Somo linapaswa kuhimiza wanafunzi wawe na moyo wa kujali maslahi ya wanadamu wengine na pia iwaonyeshe jukumu muhimu la kutekeleza katika kupambana na njaa kwa minajili yao wenyewe, familia zao, jamii zao na kwa minajili ya jamii. Njia minajili inayotumiwa kuwasilisha habari hizi kwa wanafunzi ni kupitia utalii wa hurafa na hadithi zitakazodhihirisha maadili; imani na sababu za kihalisi za kutokubali njaa na jinsi sote tunaweza kuwa mashujaa kwa kusaidia kumaliza njaa
Hurafa nyingi za kikweli na za kimasimulizi tu ni mashujaa kwa sababu ya kazi zao dhidi ya umaskini na njaa kwa kuchota malighafi ya hadithi nyingi za jamii zetu, waalimu wanaweza kutumia hurafa zao zile bora na za wanafunzi; hurafa visaasili au watu halisi kutanguliza wazo la mashujaa na kujadili sifa za shujaa kuhusiana na njaa.
Lengo 1 uliza wanafunzi kutambua watu shupavu katika historia ambao wamefanya juhudi kupafanya dunia mahali pema kwetu sisi sote na inahimiza wanafunzi kufikiria "mashujaa" wa kwao ambao wamefanya makubwa katika jamii na nchi zao. Inawasilisha wazo kuwa sote tunaweza kufanya jambo katika kumaliza njaa na ukosefu wa lishe na kwamba kila mmoja wetu, hata kwa njia ndogo anaweza kuwashujaa kwa mtu mwingine.
Lengo 2 linapendekeza hatua maalum zinazoweza kuchukuliwa na wanafunzi kupambana na njaa kwa minajili yao wenyewe, familia zao na jamii zao. Kutumia tafiti maalum kama msingi wa kuzua mawazo, wanafunzi wanahimizwa kujaribu kutumia yale waliyosoma katika jamii zao.
![]() | 1. Kujua sote tunaweza na lazima tufanye jambo katika kupambana na njaa |
![]() | 2. Kutambua jinsi tunaweza kupambana na njaa na ukosefu wa lishe bora katika jamii zetu na duniani |