Lengo 1:Kujua sote tunaweza na lazima tufanye jambo katika kupambana na njaa

Vifaa
Maelezo:
Kuhusu Siku ya Chakula Duniani duniani
Kulisha Akili, Kupambana na Njaa
Dhana:
Kila mtu anaweza kuwa shujaa katika kupambana na njaa
Yaliyomo
- Mashujaa wakuu wamekuweko katika historia. Hurafa zipo katika jamii nyingi kuhusu mashujaa wakuu ambao wamepigana dhidi ya njaa na umaskini kwa minajili ya watu maskini. Hurafa nyingi zimejikita kwenye ukweli halisi na nyingine zinahusu imani za kidini za watu fulani ingawa baadhi ya hurafa zimejikita kwenye ushindi, hurafa zinazodumu zaidi ni zile zinazohusu watu waliosaidia watu wengine dhidi ya njaa na umaskini.
-
Pamoja na hurafa, watu halisi wamebadili mkondo wa historia na kupigana dhidi ya mateso ya wanadamu na njaa katika nchi zote ulimwenguni . Wengi wa watu hawa walijitolea mhanga katika jududi za kuwasaidia wanadamu wenzao.
-
Sifa za shujaa wa kweli ni uwezo wa kimaadili, ushupavu, na kuwa na nia ya kuwasaidia watu wengine.
-
Mashujaa wa kimashirika/kiserikali: Watu wengi wamefanya kazi ili kuleta mabadiliko katika njaa katika mashirika na serikalini. Mashirika na wakala za serikali zina hazina za kutusaidia. Mamia ya vyama vimeamrishwa kufanya kazi kwa mambo tofauti ya njaa. Mashirika haya ni pamoja na vikundi vya binafsi, wakala za serikali, mashirika ya kimataifa na miungano ya kimaeneo. Baadhi ya shughuli zao zinajumlisha misaada, utafiti na utetezi: Makundi fulani huhusika tu na mataifa fulani, makundi fulani hushughulikia maeneo fulani, kama vile elimu na kilimo.
Matendo
- Mashujaa wetu ni nani? Waulize wanafunzi kuorodhesha mashujaa watatu; wawe wanaishi au waliokufa wa kikweli au wa kimasimulizi tu. Jadili sifa za mashujaa hawa wote. Jadili sifa tunazothamini sisi kama watu.
- Kutokana na orodha ya wanafunzi wa waalimu, chagua mashujaa kadhaa na viongozi ambao wamefanya kazi dhidi ya njaa, umaskini au dhuluma na maonevu na kwa kifupi eleza michango yao.
- Waulize wanafunzi hawa ikiwa mashujaa hawa ni tofauti nasi, au pia sisi tunaweza kupata sifa hizi miongoni mwetu na hivyo kupigania mabadiliko. Waulize wanafunzi ikiwa wanajua watu wowote katika jamii yao ambao wanajali na wana ushupavu wa kusaidia wengine katika hali za hatari na siku nyingine za kawaida. Waambie wanafunzi waeleze sifa za hawa watu wanaosaidia wengine katika jamii.
- Waulize wanafunzi ni kitu gani wengependa wao kufanya kusaidia jamii zao, jajii zao, au dunia. Waambie wanafunzi waandike shairi au hadithi kuhusu au kuchora picha kuhusu njaa au waulize kueleza kile watatakacho kufanya kumaliza njaa. Picha hizi na hadithi zinaweza kuonyeshwa eneo la shuleni au katika maeneo ya jamii. Hadithi zinaweza kutumwa kwa magazeti ya maeneo au ya nyumbani au kusomwa katika stesheni za redio.
- Jadili jinsi darasa lao ni moja katika madarasa ya maelefu kote ulimwenguni kushiriki katika masomo ya siku ya chakula duniani na lengo kuongeza uelewa wa njaa na ukosefu wa lishe duniani na kuhimiza watu kote duniani kuchukua hatua dhidi ya njaa. Wanafunzi kote ulimwenguni wanajifunza pamoja kuhusu jinsi wanavyoweza kufanya kazi pamoja ili kuwa sehemu ya watu wanaotaka kumaliza njaa. Soma au andika tena maelezo Kuhusu Siku ya Chakula Duniani kwa wanafunzi ili kuwafanya wajue baadhi ya juhudi za dunia ili kupambana na njaa.
-
Masomo ambayo madarasa yote yamekuwa yakitumia ni Kulisha Akili, Kupambana na Njaa, iliyoandaliwa kusaidia kupambana na Njaa kupitia elimu na habari huku ikiwa na lengo la kuhimiza kila mmoja wetu sisi kushiriki katika shughuli ya kujenga dunia isiyo na njaa. Jadili ni kwa vipi wanafunzi wanaweza kunufaika kwa kubadilishana habari walizopata kuhusu njaa na madarasa mengine katika nchi yao au kote duniani. Tuma mapendekezo haya kwa washiriki katika Kulisha Akili, kupambanana na Njaa walioorodheshwa katika utangulizi.
- Wasiliana au waeleze wanafunzi wawasiliane na mashirika ya kimataifa ambayo ni washiriki wa kimataifa ambao ni washiriki katika Kulisha Akili, Kupambana na Njaa. Baadhi ya mashirika haya yana wawakilishi wa kutoka nchi au maafisa wa miradi ya nyumbani ambao mtu anaweza kuwasiliana nao ili kuwaalika shuleni kuzungumzia kazi zao. Uliza mashirika kutuma habari kuhusu miradi yao au shughuli zao katika eneo lao kumaliza njaa na ambazo kwako wanaweza kushiriki wanafunzi darasani.
- Waeleze wanafunzi darasani wawasiliane na wengine wanaoshughulika katika mashirika ya njaa na viongozi wa kimtaa kimaeneo, wa kitaifa au wa kimataifa pia uliza kinachofanywa kuhusu kila nguzo yenye kuhimili uthabiti wa chakula (zilizojadiliwa katika sehemu zilizopita). Pia waeleze, wanafunzi watafute habari kuhusu kiasi cha njaa katika maeneo yao.
- Wasiliana na viongozi wa kimtaa na waalike darasani ili kuzungumzia hatua zipi za kienyeji zinazochukuliwa kuzuia njaa na ukosefu walishe bora. Waeleze wanafunzi wawahoji maafisa wa serikali wa sampli mbalimbali kuhusu miradi ya njaa ya mtaani. Kila mwanafunzi au kundi la wanafunzi angeweza kuandika mhutasari wa ripoti ndogo na kuiwasilisha kwa darasa.
- Waalike "mashujaa wa asili" ambao wanafunzi waliwatambua kuja darasani kuzungumzia kile wanachokifanya katika jamii kusaidia watu wengine.
- Wanafunzi wanaweza kuandika taarifa fupi kuhusu miradi yao ya njaa ya asili na kuziwasilisha ili ziweze kutiwa katika mipangilio ya siku ya chakula duniani ili kushirikiana na wanafunzi kote duniani.
