Lengo 2: Kutambua jinsi tunaweza kupambana na njaa na ukosefu wa lishe bora katika jamii zetu na duniani

Vifaa
Tafiti maalum za mradi
Dhana: Sote tunaweza kuchukua hatua kusaidia kumaliza njaa
Yaliyomo
- Hatua zinaweza kuchukuliwa katatua tatizo la njaa na lishe bora katika viwango vya jamii kitaifa, na kimataifa. Wakati mwingine hatua ni ndogo na wakati mwingine hatua hatua kubwa. Lakini jambo muhimu ni kufikiria kuhusu tatizo hili na kujua kuwa mnafanya kazi ili kupata suluhisho.
- Mkutano wa dunia wa Chakula mnamo mwaka wa 1996 zaidi ya mataifa 180 yalishiriki katika Mkutano wa Dunia wa Chakula na wote wamejitolea ili kupunguza idadi ya wale watu wasio na chakula hadi nusu ya kiwango chao cha sasa kabla ya mwaka 2015. Karatasi mbili zilikubaliwa. Azimio la Roma kuhusu uthabiti wa chakula, iliyoorodhesha mambo saba ambayo serikali zinazoshiriki zitakayofanya ili kuongeza uthabiti wa chakula, na mpango wa Mkutano wa Chakula Duniani unaonyesha malengo maalum ya kutekeleza malengo yaliyoorodheshwa katika Azimio. Mataifa yote yanayohusika yalikubali na yalitia saini taarifu, pamoja na "Tunasisitiza dharura ya kuchukua hatua sasa ili kutekeleza majukumu yetu ili kupata uthabiti wa chakula kwa vizazi vya sasa na vijavyo".
- Watu binafsi wanaweza kuchukua hatua katika kiwango cha kijamii kusaidia kumaliza njaa. Hatua hizi zinajumlisha elimu kuhusu hali ya mtaani na sera za kitaifa na masuala yanayohusu njaa, hatua mbalimbali zitakazosaidia kuleta taarifa za kibinafsi na uelewa wa kijamii kuhusu njaa. Waalimu wanaweza kusaidia kwa kukusanya habari kuhusu matatizo ya mtaani kuhusu njaa na kuuliza wanafunzi jinsi matatizo haya yanaweza kutatuliwa.
- Vijana wana nguvu na ubunifu kutatua matatizo makubwa kama vile njaa. Tafiti maalum zilizomo katika somo hili hutoa mifano ya yale ambayo yamefanywa na vijana kote duniani. Utumiaji wa tafiti maalum ni njia ya kuwapa wanafunzi matumaini na pia kuwapa mwongozo wa jinsi wao wangeweza kuleta mabadiliko duniani.
Matendo
- Mpe kila mwanafunzi au kikundi cha wanafunzi utafiti maalum (au somo tafiti maalum kadhaa kwa wanafunzi wadogo). Waeleze wanafunzi waandike muhtasari wa utafiti maalum kwa darasa na kupendekeza jinsi ambavyo mradi kama huo utafanyika katika jamii yao.
- Njaa ni tatizo la ulimwengu lakini sehemu ya suluhisho ni hatua ndogo ndogo katika kiwango cha mtaa. Baadhi ya mifano ya miradi ya ushirika ambayo imeongeza uthabiti wa chakula kwa familia na jamii ifuate. Soma maelezo ya miradi hiyo kwa wanafunzi na ujadiliane nao ni kwa vipi ambavyo miradi hiyo na migine ingeweza kutekelezwa katika kiwango cha mtaa. Vile vile jadili jinsi ambavyo miradi kama hii ingedhaminiwa.
- Wachuuzi wa Samaki wa kike nchini Burkina Faso walinunua maboksi yaliyofunikwa na kuweka kwenye baiskeli zao. Maboksi yenye barafu huwekwa kilo 10-15 ya samaki ili kuhakikisha samaki hao wanaweza kuuzwa kwa bei ya juu katika soko la mtaa.
- Wafuga nyuki katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wangeweza kununua nyuki na masega kwa pesa kidogo za mchango. Licha ya kutoa kilogram 15 za asali nyuki husambaza mbelewele kwenye miti jirani ya matunda.
- Nchini Nicaragua wakulima walipokea msaada kununua mitungi ya vyuma ili kulinda mahindi yaliyovunwa kutokana na unyevu na wadudu. Kila ghala linachukua kilogramu 550 za nafaka, inayotosheleza kulisha watu kumi kwa mwaka mmoja.
- Wanawake 40 kutoka Ghana wakulima walipewa msaada mdogo na wakanunua vifaa kutengeza vifuniko 50 vya mita moja mraba ili kulinda mbegu zao za ndizi kutokana na jua kali la Afrika.
- Kikundi cha wakulima wa Senegal walishirikiana wakanunua pampu iliyo na uwezo wa kunyunyiza hadi mita 2500 mraba za mboga kutoka kisima kilichofanywa kwa mikono.
- Chama cha ushirika kiliezeka katika mbegu za hali ya juu ili kupanda hekta 20 za kabeji, vitunguu, viazi, maua, pamoja na mbegu za kupanda nyasi za kulisha wanyama.
- Tunaweza kupata habari kuhusu njaa katika jamii zetu na duniani kutoka mahali mbalimbali tunaweza kuandika barua, tembelea watu au kupiga simu ofisini na katika maktaba (inakofikika kutafuta habari kwenye mtandao).
- Jadili umuhimu wa elimu katika kupigana na njaa. Wanafunzi wanapasawa kuhimizwa kukaa shuleni wasome iwezekanvyo kuhusu mambo ya kilimo na lishe bora, pamoja na ujuzi wa kimsingi.
- Jadili manufaa ya kazi ya huduma za jamii na kupambana na njaa na jinsi wanafunzi wanaweza kujifunza kusaidia katika eneo hili waalike wakala wa afya na maafisa wa nyanjani katika darasa kujadili idadi ya watu wanaohitajika katika kazi zinazohusiana na upambanaji na njaa.
- Waulize wanafunzi ili wakupe mawazo kuhusu hatua ambazo wao na wengine wanaweza kuchukua katika jamii zao na duniani ili kusaidia kutatua matatizo ya njaa na lishe bora. Orodhesha hatua hizo na utambue yule awezaye kuzitekeleza.
Orodha ya hatua zinazochukuliwa duniani ipo hapo chini chagua mfano mmoja au mwili kutoka katika orodha iliyoandikwa na wanafunzi au kutoka kwa orodha uliyopewa, na kufikiria jinsi matendo haya yangetekelezwa ili kupambana na njaa mtaani au duniani.
Mifano ya vitendo:
Kusaidia kuongeza utoaji wa chakula kwa kuboresha chakula na aina
tofauti ya vyakula vinavyopatikana:
- tumia bustani za jumuiya na za shuleni ili kupanga chakula
- fuga kuku na wanyama wadogo nyumbani kwa ajili ya kula au kwa biashara
- jaribu kugundua tena vyakula vilivyosahulika na vinavyostawisha katika eneo lako
- kuza mazao yaliyo bora kwa ajili ya chakula na biashara
- kuza mazao yanayositahimili udongo na maji ya eneo husika
- tumia vitendea kazi vinavyopatikana kwa ajili ya kilimo katika eneo hilo
- tafuta uwiano mzuri kati ya mazao ya biashara na chakula
- jiingize katika shughuli za shirika katika kukuza na kuuza mazao
- unga mkono wakulima wazawa; kwa kununua mazao yao
- anzisha vituo au maeneo ya kuhifadhia ya chakula cha mgao
Saidia kuweka chakula salama kwa ajili ya matumizi ya baadaye:
- weka chakula sehemu safi na salama
- weka sehemu ya maandalizi ya chakula na vitendea kazi katia hali ya usafi
- weka chakula cha ziada katika maeneo makavu, mbali na wadudu na wanyama
Wasaidie watu wote kukidhi mahitaji yao ya chakula na virutubishi:
- zifahamu hoja zako za chakula na virutubishi
- zifahamu haja mbalimbali za watu mbalimbali(hatua za maisha)
- tafuta vyakula vipatikanavyo vyenye kuleta siha nzuri
- jitolee kuhudumia maswala ya njaa
- jitolee kufanya kazi katika vituo vya usambazaji chakula.
- jenga vituo vya vyakula au maghala ya chakula ili kugawanya chakula cha ziada
- shirikiana na viwanda vya chakula ili kukisambaza tena chakula cha ziada
- waalike wakulima wa vyakula vya kuuza na wakuzaji ili wawe sehemu ya suluhisho la matatizo ya njaa katika jamii.
Jifunze kuhusu vyakula, lishe na njaa na kuyatoa maarifa na mawazo kwa wengine:
- jifunze kuhusu mfumo wa chakula katika eneo lako
- fahamu ni nani katika jamii yako wanajitahidi kupambana na njaa, wasikilize, na kubadilishana mawazo nao
- fahamu ni nani katika jamii wana maarifa kuhusu afya na kubadilisha mawazo nao
- chukua habari nyumbani kwa familia na majirani
- badilishana ripoti na miradi ya shule katika maeneo ya kijamii
- badilishana mawazo na viongozi katika jamii na taifa
- wahimize viongozi wa jamii na watoa huduma (madaktari / wauguzi / wafanyakazi wa hospitali / waktubi) kushiriki katika miradi ya shule inayohusu maswala ya njaa na lishe.
Muhtasari
Katika masomo matatu katika mwongozo huu, ambao kimsingi uliandaliwa kwa Siku ya Chakula Duniani, 16, Oktoba 2000, tumejishughulisha na matatizo ya njaa duniani. Lengo la siku ya Chakula Duniani ni kuwa na dunia isiyo na njaa haraka iwezekanavyo katika kikwi kipya. Mamilioni kati yetu leo hawana chakula cha kula kuna lazima tuweze kuelewa ni kwa nini hali hii iko hivi.
Vijana wana ubunifu na nguvu za kutatua matatizo makubwa kama njaa. Sote tukishirikiana katika mwono wa dunia isiyo na njaa, kuwa na imani kuwa hata sisi tunaweza kuleta mabadiliko, habari kuhusu hatua za kuchukua kusuluhisha na kuwa tayari kuchukua hizo, tunaweza kusuluhisha changamoto kubwa hii ya kulisha watu wote duniani na vijana wetu ambao wamerithi tatizo la njaa katika dunia yetu, itakuwa kitu cha kutuonyesha jinsi ya kupata suluhu.
Kwa kujiunga na Foramu ya KAKN, bonyeza HAPA.
