Somo 1 : Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora ni nini? Na ni Nani Aliye na Njaa?

Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45-60, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.

Taarifa kwa waalimu

Inafaa wanafunzi kuelewa kwamba chakula chenye virutubisho vya kutosha ni vya kimsingi kwa afya nzuri, ukuaji na ustawi na kwamba njaa na ukosefu wa lishe bora ni matatizo makubwa yaliyo tisho ya muda mrefu kwa afya bora ya watu, mataifa na ulimwenguni.

Lengo 1 linatoa maelezo sahili ya dhana za kimsingi za lishe na mahusiano yao kuhusu njaa na ukosefu wa lishe bora. Wanafunzi huenda wameshajifunza au bado hawajifunza lishe bora. Hii ni fursa ya ama ya kuangazia tena au kutanguliza dhana ya kimsingi ya lishe bora na kujadili jukumu la chakula mwilini. Chakula kinaangaliwa kama chenye umuhimu kwa maisha, ukuaji na ustawi na kazi kamili ya kimsingi kama vile kupumua na mzunguko wa damu. Chakula pia hutoa nguvu za kuchapa kazi,kujifunza nakucheza. Michango ya virutubishi vinaelezwa kwa njia sahili isiyotumia mtindo wa kitaalamu, dhana pevu zaidi za lishe zinaweza kutangulizwa inapofaa. Rasilimali zaidi ni pamoja na elimu ya habari ya lishe na maelekezo ya maakuli yaliyoandaliwa na shirika la Chakula na Kilimo (FAO) Shirika la Afya Duniani (WHO) na mataifa tofauti.

Lengo 2 linatoa data kuhusu njaa ulimwenguni kote na kusaidia wanafunzi kutambua maeneo yenye kuhitaji zaidi.

Lengo 3 linatambua makundi maalumu ambayo yanakumbwa na matatizo makubwa zaidi ya njaa na ukosefu wa lishe bora, na kutambua walio katika matatizo ya kiafya. Habari zaidi zinazotoa maelezo kijumla ya hali ya sasa duniani yanapatikana katika "Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora Duniani" katika Utangulizi.

Lengo:

1. Kuelewa matokeo ya njaa na ukosefu wa lishe bora
2. Kujua kiwango cha njaa ulimwenguni leo
3. Kujua ni nani aliye na njaa na aliyekosa lishe bora duniani