Lengo 1: Kuelewa matokeo ya njaa na ukosefu wa lishe bora

Vifaa

Karatasi ya Ukweli:

Chakula hutupa...

Vitamini na madini


Dhana: Chakula cha kutosha ni muhimu kwa maisha biabia na yenye afya

Yaliyomo
Matendo

Dhana:Afya mbaya, ukuaji mbaya na ustawi mbaya hutokana na njaa na ukosefu wa lishe bora

Yaliyomo

Matokeo makubwa ya kiafya na lishe hutokana na chakula haba na lishe mbaya hii ni pamoja na:

Hatari kuu za kiafya zinazohusishwa na ziada za maakuli ya lishe iliyopita kiasi ni pamoja na ugonjwa wa vifereji moyo, kupooza, kunenepa kupita kiasi na kisukari. Matatizo haya yanazidi kuongezeka katika mataifa yanayoendelea na yaliyoendelea.

Uchafu wa vyakula ni kikwazo kikubwa kwa afya ya maakuli. Watoto hasa wamo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa yanayohusiana na chakula,ambayo huwaondolea virutubishi muhimu kutokana na kuhara.

Matendo

Karatasi ya ukweli Vitamini na Madini hutoa maelezo kuhusu mojawapo ya virutubishi nane vya kimsingi au vikundi vya virutubishi na jukumu lao mwilini, dalili za kudhoofika na vianzo vyakula. Chagua kirutubishi kimoja au viwili (au vingi kadiri wakati utakavyoruhusu) ambavyo huenda vina matatizo katika eneo lako, eleza virutubishi na dalili za kiafya zilizoorodheshwa katika karatasi ya habari kisha waambie wanafunzi kueleza viini vya vyakula vya kirutubishi kinachohusika. Waambie wanafunzi wapendekeze njia ambazo huenda zikawawezesha watu kupata virutubishi zaidi katika mlo wao. Ili kubainisha matatizo mahususi ya virutubishi katika eneo lako, wasiliana na afisa wa afya katika eneo lako au wa nyanjani au Idara ya Afya.


Dhana:Njaa huathiri afya nzuri ya watu, mataifa na ulimwengu

Uwezo wa nchi unategemea uwezo wa watu wake. Watu wakiwa na afya, wenye nguvu na siha nzuri, huwa wana nguvu, ubunifu, usalama na moyo wa kufanya kazi, kusuluhisha matatizo na kuishi maisha yao ya kila siku kwa hesima na furana na hatimaye kuendeleza ustaarabu hadi viwango vya juu. Wananchi waliolishwa vyema ni wazalishaji ambao wanaichangia jamii yao. Watu ambao hawana siha nzuri hawana nguvu za kufanya kazi au kujifunza na aghalabu wanahitaji huduma za afya mara kwa mara. Gharama za njaa kwa njia ya uwezo uliopotea, huduma za afya na uwezekano wa misukosuko ya kijamii huweza kuifadhaisha jamii.

Matendo

Jadili maswala yaliyoorodheshwa hapo juu pamoja na wanafunzi. Pamoja na hao wanafunzi, unda orodha ya watu mashuhuri katika jamii yao, nchi yao,au ulimwenguni, wawe wa zamani au wa sasa, ambao wamesaidia kuijenga dunia bora. Michango yao inaweza kuwa na kijamii au ya kiutu, au kupitia ubunifu wa kisayansi au kisanii. Wanashauri wanafunzi kuitafakari tofauti ambayo ingekuwepo iwapo watu wangekuwa na ukosefu mkubwa na lishe bora, wenye njaa au wagonjwa wasioweza kufanya kazi wanazizozifanya. Waeleze jinsi ilivyo muhimu kwetu sote kuwa kila mtu ulimwenguni aweze kuutumia uwezo wake kadiri awezavyo. Uwezo uliopotea unatuumiza sote.




Lengo 2. Kujua kiwango cha njaa ulimwenguni leo
Lengo 3. Kujua ni nani ana njaa na ukosefu wa lishe bora ulimwenguni