Lengo 2: Kujua kiwango cha njaa ulimwenguni leo
Vifaa
Picha: Ramani ya njaa Duniani
Global Information and Early Warning System on Food and Agriculture (GIEWS)
The state of food insecurity in the world
Dhana :Licha ya ustawishaji mkubwa, mamilioni ya watu hii leo wana njaa na wanakosa lishe bora
Yaliyomo
- Idadi ya watu ulimwenguni inaendelea kuongezeka kwa kasi mno. Katika mwaka 1999, kadirio rasmi la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu ulimwenguni linaonyesha kuwa kuna zaidi ya watu bilioni sita. Tutashuhudia ongezeko zaidi la watu bilioni 2 katika kipindi cha miaka 25 ijayo, kiasi kikubwa kikiwa kutoka nchi ambazo hivi sasa zina matatizo makubwa ya kuwalisha watu wake.
- Ingawa idadi ya watu ulimwenguni iliongezeka kwa kasi mno(kwa zaidi ya asilimia 70) katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, maendeleo makubwa yamepatikana katika kuongeza wingi na ubora wa usambazaji wa chakula ulimwenguni na vilevile kuboresha hali ya lishe ya watu.
- Katika ulimwengu unaoendelea, ambapo idadi ya watu imekaribia kuwa maradufu katika kipindi hiki, sehemu ya kiasi cha watu wanaoishi katika hali mbaya ya utapiamlo imepunguzwa kwa nusu (kutoka asilimia 36 hadi18 katika 1995-1997)
- Hata hivyo, watu milioni 790 - moja kwa watano katika nchi zinazoendelea - bado hawana chakula cha kutosha kukidhi mahitaji yao ya kila siku ya lishe. Maendeleo hayajawanufaisha watu wote; wakati baadhi ya nchi zimepata maendeleo makubwa, njaa imeongezeka katika nchi zingine, hasa zile ambazo tayari zina matatizo makubwa kuwalisha watu wake.
- Uwezo wa kufikia hifadhi za vyakula bora anuwai, na salama ni tatizo kubwa katika nchi nyingi, hata pale ambapo kuna chakula cha kutosha katika kiwango cha kitaifa.
Matendo
- Onyesha picha ya Ramani ya njaa Duniani, ambayo inaonyesha maeneo yaliyo na matatizo makubwa ya njaa na ukosefu wa lishe bora. Eleza jinsi ramani hiyo inavyoonyesha maeneo ambapo watu wengi hawapati vyakula vyote wanavyohitaji kula. Onyesha maeneo yenye idadi kubwa ya watu wenye njaa. Eleza kwamba nchi zote zina baadhi ya watu walio na njaa.
- Onyesha eneo lako/eneo la ulimwengu, na ujadili kiwango cha matatizo ya njaa katika eneo lako ukilinganisha na maeneo ya karibu na ulimwengu kwa jumla.
