Vitamini na Madini

Vitamini na madini hujulikana kama virutubishi vidogo. Huhitajika katika viwango vidogo zaidi kuliko protini, mafuta na wanga lakini ni muhimu kwa lishe bora. Husaidia mwili kufanya kazi vizuri na kuwa na afya. Baadhi ya madini pia huwa vijenzi vya tishu, kwa mfano, kalsiamu na floridi katika mifupa na meno nayo chuma hupatikana katika damu.

Ayani ni kijenzi kikuu cha seli nyekundu za damu na ni muhimu katika kusaidia seli za mwili kuendelea kufanya kazi vizuri. Anemia ni uhaba wa ayani ndilo tatizo lililosambaa sana ulimwenguni. Inaweze kuwa mbaya kwa watoto na wanawake wa umri wa kuzaa, hasa wakati wa uja uzito, lakini pia huathiri wanaume na wanawake wa umri mkubwa. Husababisha utepetevu (utenda kazi mdogo), matatizo ya usomi, ukuaji mbaya na ustawi, na ongezeko la ugonjwa na vifo kwa akina mama, hasa wakati wa kujifungua. Viini bora vya ayani ni nyama, samaki, kuku, ini na viungo vingine vya nyama. Ayani pia hupatikana kwenye kayamba (vyakula vya jamii ya kunde), mboga za majani kijani kilichokolea na matunda yaliyokaushwa, lakini ayani hii haisharabiwi vizuri na mwili kama ilivyo ayani itokanayo na vyakula vya wanyama. Kuongeza utumiaji wa vitamini C pamoja na ayani kutokana na mboga huwezi kusaidia ayani zaidi kuingia mwilini na kutumiwa vizuri.

Vitamini A huhitajika kwa ajili ya kujenga na kudumisha tishu zenye afya mwilini kote, hasa macho, ngozi, mifupa na tishu mishipa ya kupumua na kumeng’enya. Pia ni muhimu sana kwa kufanya kazi kwa mfumo wa kinga. Ukosefu wa vitamini A huweza kusababisha kutoona vizuri usiku, vidonda vikali vya macho na, katika hali mbaya zaidi, upofu wa kudumu. Haya huwakumba hasa watoto wenye utapiamlo, hasa walio na surua na maambukizo mengine. Ukosefu wa vitamini A huweza pia kusababisha ongezeko la ugonjwa na kifo kutokana na maambukizo. vitamini A hupatikana tu kwa kawaida katika vyakula kutokana na wanyama, hususa maziwa ya kukama, ini, mayai na vyakula vingine vya kila siku. Hata hivyo matunda na mboga zenye rangi nyeusi huwa na karotini ambayo mwili hubadilisha kuwa vitamini A. Vyakula vyenye wingi wa vitamini A ni pamoja na karoti, viazi vitamu vya njano iliyokolea, maembe na mapapai.

Thiamini, riboflauini, niasini, vitamini B6, tolati, asidi ya pantotheni, vitamin B12 na biotini huwa katika kundi ambalo wakati mwingine hujulikana kama vitamin B changamano. Vitamini B huwa muhimu katika kubadilisha kabohidrati, shahamu na protini kuwa nguvu na kuwa kuzitumia kujenga na kukarabati tishu za mwili. Uhaba wa vitamini hizi huweza kusababisha athari kubwa zikiwemo udhaifu wa misuli, kupooza, kuchanganyikiwa kiakili, kasoro ya mfumo wa neva, matatizo ya kumeng’enya, ngozi yenye kupasuka na kubambuka, anemia kali na mshtuko wa moyo.

Foleti (asidi jani, folasini) huhitajika katika kutengeneza seli nyekundi zenye afya na ukosefu wake ni chanzo kikuu cha anemia miongoni mwa wanawake na watoto wadogo. Ukosefu wa foleti wakati wa ujauzito huweza kusababisha kasoro za uzazi. Utumiaji wa mara kwa mara wa vitamini B - ni muhimu. Vyakula vyenye vitamini B - ni mboga za kijani, njugu, maharagwe, mbaazi, nafaka, nyama, samaki na mayai.

Vitamini C huhitajika ili kuongeza utumiaji wa kawaida wa ayani, kutengeneza kolajeni (tishu ya kuunga) ambayo huziunga seli za mwili pamoja, na kutumika kama kiondoa uokisidishaji. Ukosefu wa muda mrefu wa vitamini C huweza kusababisha ugonjwa wa kuvimba ufizi na kutoka damu (kiyeye). Dalili za ugonjwa huu ni ufizi wenye uchungu kutoka damu, vifundo vilivyovimba, na huweza kufisha. Matunda mengi, hasa sitriki na mapera, na aina nyingi za mboga, pamoja na viazi, ni viini vizuri vya vitamini C. Kula matunda freshi na mboga fresh ni muhimu kwa watu wazime na watoto.

Vitamini D ni muhimu hasa kwa mwili kutumia kalsiamu. Vitamin D hupatikana katika mafuta ya samaki , mayai na maziwa na vile vile kutolewa na mwili wakati ngozi inapokuwa wazi juani. Ukosefu wa vitamini D husababisha nyongea (chirwa), ugonjwa ambao husababisha mifupa ya watoto wadogo kuwa mnyororo na kulemaa.

Kalsiamu na fosforasi ni muhimu kwa utunzaji wa mwili na kuwa na mifupa imara yenye afya na meno. Maziwa na bidhaa nyingine za maziwa ni viini mwafaka vya kalsiamu na fosforasi.

Ayodini ni muhimu kwa ukuaji mzuri na ustawi. Ukosefu wa ayodini katika maakuli husababisha tezi na matatizo ya kiakili. Ayodini hupatikana kwenye vyakula vya baharini na katika vyakula vinavyopandwa kwenye mchanga wenye wingi wa ayodini. Katika maeneo ambapo mchanga una viwango vya chini vya ayodini, hatua zinafaa kuchukuliwa kuongeza ayodini kwenye vyakula, kwa kawaida kupitia kwa chumvi yenye ayodini.