Asia

Kipindi cha ukuaji wa haraka wa uchumi kimeleta faida kubwa katika uthabiti wa chakula katika sehemu kubwa ya Asia na Pasifiki. Nchini Cambodia ambapo kiwango cha watu wenye lishe isiyo nzuri kilipungua kutoka 62 hadi 33 kati ya 1980 na 1996 waliongoza njia. Nchi nyingi katika eneo hili zilidhihirisha kupungua kwa idadi hii zikiwemo China, India, Indonesia, Myanmar, Nepal, Pakistan na Vietman. Hali ya lishe isiyo nzuri iliongezeka katika nchi mbili - Mongolia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea. Katika Korea iliongezeka kutoka asilimia 16 hadi 48. Japo maendeleo ya kifedha yamekuwa mabovu katika mataifa fulani lakini maendeleo ya kijumla ni mazuri.

Cambodia - yavuna matokeo ya amani

Mashamba mengi yanalimwa, chakula kingi kinazidi kuzalishwa na ni watu wachache sana walio na njaa nchini cambodia, huku nchi ikitoka kwenye miongo mingi ya mizozo. Baina ya 1970 na 1996 wakulima walikaribia kulima maradufu eneo walilokuwa wakipanda chakula. Mavuno ya mchele ambacho ni chakula cha msingi cha Cambodia yalioongezeka kwa asilimia 64. Uzalishaji wa Nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe na kuku uliongezeka kwa haraka. Kwa sababu ya ongezeko la chakula, watu wa Cambondia hula vizuri hata kama idadi ya watu imezidi kukua na uagizaji wa chakula umekwenda chini.

Licha ya maendeleo haya ya karibuni, Cambodia ni nchi maskini na watu wake wengi hawana uthabiti wa chakula. Hata baada ya ongezeko la asilimia 21 tangu 1980 chakula cha Cambodia cha wastani hakiwezi kutosheleza mahitaji ya chakula ya kimsingi. Zaidi ya thuluthi moja ya watu wake ni maskini. Umaskini wa nchi hiyo unahusishwa na ukosefu wa sampuli katika ulaji wa watu wake. Asilimia 80 ya chakula chao cha kutoa nguvu ni mchele.

Miongo ya vita iliathiri vibaya mifumo na mitambo ya unyunyuziaji. Mashamba mengi yameachwa huku ndani mwake mkiwa na mabomu. Mwafaka wa amani wa 1979 ulifungua milango ya maendeleo; marekebisho ya kiuchumi yaliyoanzishwa mnamo 1992 yalidhibiti mfumko wa bei . Wakulima kwa upande wao wakaongeza kiwango cha mashamba yaliyolimwa na kuongeza uzalishaji wa mchele na pia kuongeza kilimo cha mimea mingine na ufugaji wa wanyama wa mauzo katika nchi za nje.

Miradi ya kutoa mabomu na kurekebisha mifumo ya unyunyizaji inaendelea . Kuna mradi ulioanzisha kazi kwa makundi hasiriwa.

DPR Korea - Mavuno mabaya

Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Korea imeathiriwa vikali na mafuriko, ukame, na kuvunjika kwa mahusiano na China na Muungani wa Kisovieto katika miaka ya 1990. Matokeo ya hali hii yamekuwa mabaya hasa kwa utoaji wa chakula na kwa hali ya lishe kwa watu wake. Uzalishaji wa nafaka ulishuka kwa kiwango chini ya nusu ya utoaji wa 1980, huku kiwango cha watu walio na lishe mbaya kikiongezeka hadi kufikia nusu ya idadi ya watu wake.

Kuanguka kwa uchumi kulifanya nchi isiwe na pesa au uwezo wa kukopeshwa ili kulipia vyakula vya kuagiza. Msaada mkubwa ulitolewa lakini matatizo ya utendaji yalifanya chakula kisifikie watu wote waliokihitaji. Tatizo hili liliathiri mfumo wa kitaifa wa ugawaji kwa kiwango kibaya sana.

Mfumo huu unauza vibaba fulani maalum vya mchele na mahindi kwa wakazi wa mjini na kwa watu wanaofanya kazi katika mashamba ya serikali na biashara katika sehemu za mashambani. Wakati mazao yaliposhuka na viwango vya chakula cha kuagizwa kikishuka vile vile chakula cha akiba hakingeweza kulisha watu inavyostahili. Vibaba vilipunguzwa kwa kiwango kikubwa na watu wengi wakapunguza utumiaji kwa kiwango kikubwa.

Kuanguka kiuchumi kulifuata onyounyo ustwai mkubwa wa kiuchumi. Huku nchi ikiwa na mashamba machache ya kilimo na kipindi kifupi mno cha upanzi, faida ilikuwa imepatikana kwa sababu ya kilimo cha hali ya juu. Mara nchi haikupata vipuli, mbolea, dawa za wadudu na maji ya mabomba kwa hivyo mazao yalipungua kwa kiwango kikubwa. Kuanzia 1995 miaka miwili ya mafuriko ilifuatiwa na kiangazi kikubwa kiliathiri mashamba makubwa na mimea. Nchi hii sasa inajaribu kuimarisha mazao ya kilimo kwa kutumia mbegu bora, kurekebisha mifumo ya unyunyiziaji wa mashamba maji, kuboresha rutuba ya udongo na njia ya upanzi kuwili.