Nchi nyingi katika eneo la Mashariki ya karibu na Kaskazini mwa Afrika zimekuwa na mafanikio makubwa na kupunguza viwango vya matatizo ya lishe. Kwa kweli eneo hili lina nchi kumi miongoni mwa nchi 14 zinazoendelea ambapo matatizo ya lishe yanaathiri chini ya asili mia 15 ya idadi ya watu.
Maendeleo ya Morocco ambapo kiwango cha matatizo ya lishe kilishuka kutoka asilimia 10 hadi 5 iliwakilisha ukuaji katika kikundi hiki cha nchi zenye maendeleo mazuri. Ongezeko kubwa zaidi lilikuwa Afghanistan ambapo watu wenye lishe mbaya waliongezeka kutoka asilimia 33 mnano 1980 hadi asilimia 62 mnamo 1996, na Iraq ambapo kiwango kiliongezeka kutoka asilimia 4-15 katika kipindi hicho cha mwaka.
Huku wakiwa na utajiri wa madini na nafasi bora kama kituo cha biashara na mauzo, Morocco imekuwa na maendeleo mazuri ambayoyamepunguza hali ya lishe mbaya kwa viwango vidogo. Baina ya 1980 na 1966 chakula cha kila siku kiliongezeka kutoka kalori 2,723, hadi kalori 3186 na kiwango hiki kilifikia viwango sawa na baadhi ya mataifa yaliyoendelea. Mafanikio yalitokana na utoaji wa chakula na ule wa viwanda. Uzalishaji wa nafaka na viazi uliongezeka zaidi ya maradufu hali hii iliwezeshwa na ongezeko la mazao pamoja na eneo lililokuwa limelimwa. Chakula kingi katika kile kilichozalishwa kilitumika kwa malisho, huku uagizaji pia ukiongezekai ili kukidhi mahitaji ya chakula. Huku uchumi ukikua kwa kiwango cha asilimia 4 kila mwaka Morocco imeendelea kuwa jiji. Kumekuwepo na maendeleo katika uchukuzi, usafi na elimu katika miji. Hata hivyo nusu ya idadi ya watu wako katika sehemu za mashambani ambapo kuna umaskini uliokita miongoni mwa wakulima wa jadi na wafugaji. Nusu ya idadi ya watu haina maji ya kutosha na safi na asilimia 56 hawakusoma. Kuna matatizo mengi ya mazingira. Maji ya kilimo na ulishaji wanyama si rahisi kupatikana na asilimia 61 ya ardhi imeharibiwa ili kumaliza njaa katika maeneo yaliyobakia. Itabidi hatua madhubuti zichukuliwe ili kuwa na kilimo chenye maendeleo na kuzalisha kazi na pato katika sehemu za miji.
Uzalishaji wa vyakula na uwepo wa chakula vimeathiriwa na miongo ya vita nchini Afghanistan. Uzalishaji wa nafaka ulishuka wakati wakimbizi walipoongeza idadi la watu asilimia 25 baina ya 1980 na 1996. Kwa sababu hiyo chakula cha kila siku kwa wastani kilishuka kutoka kalori 2186 hadi 1710 . Hiki ni kiasi kilicho chini ya mahitaji ya kimsingi. Thuluthi mbili za mikoa ya nchi zina matatizo ya ukosefu wa chakula, lakini uchumi huu ambao umo katika vita hauwezi kuwa na chakula cha kuagiza cha kujaza pengo hilo.
Hali ya Afghanistan ni ya kipekee maana Afghanistan ipo katika eneo ambapo hali ya utapiamlo iko chini. Lakini ni mfano wa nchi zilizoathiriwa na vita na kwa hivyo zilizo katika hali ya kutolewa misaada ya aina mbalimbali. Zaidi ya asilimia 40 ya sehemu ya kilimo katika nchi hiyo zimejaa mabomu na kwa hivyo haziwezi kulimwa. Maelfu ya watu waliotegemea kilimo wamehamia miji na miji mikuu, ambako wamejumuika na wakazi wa miji waliomaskinika. Ni asilimia 15 ya idadi ya watu walio na maji safi na asili mia 70 ni watu wasio na elimu. Mapigano ya mara kwa mara na vizuizi kuhusu usafiri ni katika mambo yanayozuia ujenzi wa nchi.
Katika watu 50 nchini Afghanistan mmoja ameathiriwa na bomu. Kila siku kuna milipuko ya mabomu inayoua au kulemaza watu kumi zaidi ambao thuluthi yao ni watoto na wanawake. Watu wengi walioathiriwa na vita au mabomu hawawezi tena kufanya kazi. Watu hawa wanakuwa ni wa kutegemea familia zao, jambo ambalo linawapa uzito katika kuwalisha na kuwaangalia. Chakula kingi cha msaada hata hakitoshelezi mahitaji ya kimsingi ya watu wengi wenye utapiamlo. Kutakapopatikana amani hakuna matumaini ya kupata suluhu za kudumu.