Huku zikiongozwa na Ghana, nchi nane Afrika Magharibi zilipunguza njaa kwa kiasi kikubwa baina ya mwaka wa 1980 na 1996. Yafaa ieleweke hasa kuwa zile nchi tano zilizopiga hatua kubwa kwenye shughuli hii ulimwenguni kote, zote ni kutoka eneo hili. Hali hii hata hivyo ilikuwa kinyume sana Afrika ya Kati ya Mashariki, na ya Kusini. Katika maeneo haya viwango pamoja na idadi ya watu wenye utapiamlo iliongezeka hasa. Ni nchi ya Burundi iliyokuwa na viwango pamoja na idadi kubwa zaidi ya watu wenye utapiamlo, ambapo viwango vya watu wenye utapiamlo, vilipanda kutoka asilimia 38 hadi asilimia 63 baina ya mwaka wa 1980 na 1996. Hata hivyo nchi nyingine 13 katika Afrika ya Kati, ya Mashariki na ya Kusini pia zilionyesha ongezeko hili.
Ikiwa na uchumi uliomarika na nyongeza zisizotarajiwa za vyakula vya msingi, Ghana ilipunguza hali ya lishe isiyo bora haraka zaidi ya nchi nyingine yo yote ile ulimwenguni baina ya mwaka wa 1980 na 1996. Kwa wastani , ulaji wa chakula uliongezeka kutoka kalori 1,790 hadi zaidi ya kalori 2,600 kwa siku. Manufaa haya yalitokana hasa na uzalishaji vyakula ulioongezeka, huku vile vilivyoagizwa kutoka nje vikibakia vivyo hivyo. Kuleta sampuli za mihogo zilizokuwa zimepiga hatua katika ustawi kulisaidia kuongeza mazao ya hiki chakula msingi kwa asilimia karibu 40. Mazao ya viazi vikuu, mahindi, na mchele pia yaliongezeka sana, na uchumi huo kabambe uliwatia moyo wakulima kuongeza eneo la upandaji mimea kwa asilimia iliyozidi 25.
Kimsingi uchumi ulikua kwa asilimia ya 2.3 kwa mwaka . Mafanikio haya yalisababisha ukuaji na uendelezaji katika nyanja za usafi, afya na elimu. Idadi ya watu waliopata maji safi na salama iliongezeka kutoka asilimia 35 hadi 654. Kutokujua kusoma na kuandika kulipunguzwa sana, kutoka asilimia 57 hadi 36.
Kipindi hiki cha ukuaji wa haraka nchini Ghana kilianzishwa na mageuzi yaliyolenga katika kuupa uchumi wake nguvu baada ya kipindi kirefu cha mporomoko wa uchumi. Mpango spesheli wa kusimamia Madhara ya Kijamii kuhusiana na Marekebisho pamoja na mipango mingine ya kijamii ulisaidia kuyakinga makundi yaliyoathirika kutokana na athari zo zote mbovu ambazo zingetokea kwa sababu ya mageuzi.
Ijapokuwa Ghana ilipiga hatua hii kubwa, Karibu thuluthi moja ya wananchi wake bado ni maskini, asilia 10 ya watu wake yaishi katika hali za umaskini uliokithiri vijijini. Viwango hivi vikubwa vya umaskini vinamaanisha kuwa usalama wa chakula haupo mbali na ukweli kuwa kunavyo vikundi vinavyoathiriwa bado. Itafaa ukuaji wa uchumi uendelee huku nafasi za watu wa kuajiriwa katika sekta zisizo za mashamba zikindelea ili kudumisha viwango vya maendeleo.
Utapiamlo umeongezeka sana na uzalishaji chakula umepungua huku Burundi ikiwa yapambana ili kukabili idadi inayoongezeka ya watu, uharibifu wa ardhi, na mizozano ya kikabila. Kwa wastani ulaji wa chakula ulipungua baina ya mwaka 1980 na 1996 kutoka kalori 2020 hadi kalori 1669, hali iliyokuwa chini ya matarajio. Uzalishaji wa mihogo, viazi vitamu na maharagwe ambavyo ni vyakula msingi vya Waburundi ulipungua pia.
Ikiwa na kiwango cha wastani cha ukuaji wa mwaka cha asilimia 2.7, idadi ya watu wa Burundi imekuwa ikiongezeka kwa kasi sana kuliko uchumi wake, hali ambayo imezalisha viwango vya ukuaji vilivyo kinyume kwa kila mtu. Uchumi hafifu wa Burundi na kutengwa kwake kijiografia ni vitu ambavyo vimeifanya nchi hii kuwa ya mashambani sana (ambapo asilimia 90 ya watu wake waishi mashambani) na ambayo inategemea hasa uzalishaji vyakula nyumbani.
Ukuaji kasi wa idadi ya watu umetanua rasilmali ndogo za ardhi zilizopo. Zaidi ya asilimia 80 ya ardhi ya Burundi na ambayo ni ya milimamilima na inayoweza kuvunjika kirahisi, imeharibika sana. Nyanja zinazolimwa na zile zilizo na mazao ya mimea zimekuwa zikipungua.
Matatizo ya uzalishaji ya Burundi yameongezwa na hali za usafiri pamoja zile za vifaa vya mauzo. Pia mizozano ya kikabila imevuruga uzalishaji, mali na kubana zaidi nafasi za biashara.
Kutengwa kwa Burundi kunaifanya iwe na matatizo kibiashara na imezuia ukuaji wa sekta zisizo za kilimo, lakini hali ya ukuaji wa idadi ya watu, kuharibiwa kwa mazingira na kushuka kwa uzalishaji wa kilimo inaonyesha kuwa suluhu ya uthabiti wa chakuka kwa Burundi lazima itafutwe katika sekta isiyo ya kilimo.