Viwango na mikondo ya lishe isiyo nzuri havilingani katika Amerika Kusini na Caribbean. Katika nchi nyingi za kusini mwa Amerika viwango hivi tayari viko chini au vinazidi kudidimia. Katika Amerika ya kati, kwa upande mwingine viwango vinaongezeka katika nchi nyingi, hata kama Honduras ilipata mafanikio kwa kupunguza kiwango cha lishe isiyo nzuri kutoka asilimia 31 hadi 21. Katika nchi ya Caribbean , Cuba kulikuwa na watu wa lishe isiyo nzuri walioongezeka kutoka asili mia 3 hadi 19, na wakawa kwa njia nyingi kama majirani zake waliokuwa na ongezeko la lishe isiyo nzuri tangu mwaka 1980.
Ukuaji thabiti wa kiuchumi, pamoja na misaada ya kutosheleza kwa raia wake maskini zaidi, imesaidia Honduras kupunguza watu wake walio na matatizo ya lishe isiyo toshelezi. Ongezeko katika uzalishaji, uagizaji na utumiaji wa akiba vyote vilisaidia kuwapa chakula raia wa Honduras. Uzalishaji wa mahindi ulikaribia marudufu baina ya 1980 na 1996. Ongezeko jingi halikuliwa na watu bali na wanyama waliofugwa katika kilimo cha Wanyama kilichofana. Ulaji wa mahindi na watu kwa hakika ulipungua kiwango mafuta yaliyotokana na mboga na sukari vilivyomiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na ulaji wa nyama na pia maharagwe vilichangia viwango vikubwa vya ulaji.
Kwa kuwa Honduras walianzisha programu ya urekebishaji mnamo 1988, uchumi wa nchi umekua kwa kiwango cha asilimia 2.7 kwa mwaka . Maendeleo na ufanifu umesaidia kuleta maji safi kwa asilimia ya watu 87 ya raia wake. Usaidizi kwa raia unatolewa kupitia Huduma ya Akiba ya Kijamii (Social Investiment Fund) ambayo imefikia mafukara wengi. Mradi wa chakula unatoa kadi kusaidia watoto wa shule, Mama na Wazee kununua chakula na vitu vingine vya kimsingi.
Licha ya mafanikio ya hivi majuzi Honduras ina changamoto kubwa ukuaji wa uchumi haujaondoa tofauti kubwa katika mapato. Umaskini na kutokuwepo kwa chakula ni hali ambayo ipo. Nusu ya watu wa Honduras wanaishi mashambani . Huko mashambani karibu asilimia 40 wanaishi katika hali ya ufukara, huku watu wengi wakifanya kazi katika mashamba makubwa. Kilimo cha kibiashara kinatoa nafasi nzuri kwa mauaji hat ahivyo kuona changamtoto ya kungawa manufaa yanayo patikana.
Cuba imekuwa na matatizo ya kushuka kwa uchumi na viwango vya lishe isiyotosheleza vimeongezeka baada ya kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti. Kilimo chake kilijikita katika uzalishaji wa bidhaa za uuzaji katika mataifa ya nje. (hasa sukari na tumbaku) Katika hali hii Cuba ilikuwa imefaulu katika kupunguza lishe iliyo toshelevu. Kwa viwango vya chini na kutegemea chakula cha kuagiza cha kiwango kilicho zaidi ya nusu.
Wakati ambapo Cuba iliacha biashara yake na Muungano wa Kisoviet chakula cha kila siku kilishuka kwa kiwango cha zaidi ya kalori 500 kwa kila mtu, hasa kwa sababu ya kushuka kwa kiasi kikubwa katika chakula cha kuagiza. Uzalishaji wa vyakula vingine pia nao ulishuka kwa sababu ya mbolea ya kuagiza, lakini Cuba iliweza kuzalisha kiwango karibu sawa kwa kutumia sehemu kubwa zaidi ya ardhi.
Kushuka kwa uchumi kumeongeza idadi ya watu wanaotegemea usaidizi huku uzalishaji ukiwa imeshuka kwa wafanyikazi wengi na familia zao. Kuzuiwa kwa biashara na Marekani kumezidi kuongeza matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo.
Licha ya matatizo yake ya hivi karibuni, Cuba ni moja katika nchi zilizoendeleza na kulisha vyema ukilinganisha na nchi nyingine za Caribean na Amerika Kusini. Zaidi ya nusu ya njia za nchi zimetiwa lami na asilimia 95 ya watu wana maji safi.
Tangu 1993, serikali ya Cuba imetilia mkazo uzalishaji wa chakula na kuviunda upya.
Dalili zinazojitokeza zaonyesha kuwa muundo mpya wa uchumi unakua na masoko yameanza kurudia katika hali yake. Hata hivyo maendeleo ya mpito yanaonekana kuwa mbali kukamilika.