Lengo 1: Kuelewa mfumo wa chakula unaolisha watu
Vifaa
Jedwali: Jedwali ya Mfumo wa Chakula
Dhana :
Mfumo unaotoa chakula ni tata
Yaliyomo
-
Hatua zinazohusika katika mfumo wa chakula ni pamoja na:
- Kujiandaa kupanda chakula
- Kupanda chakula
- Kukitoa chakula shambani
- Kuchambua,kuuza au kukiweka chakula.
- Kuandaa na kukila chakula.
- Kila moja ya hatua hizi inahusisha hatua nyingi na maamuzi (Jedwali ya Mfumo wa Chakula). Na kila hatua huweza kuhusisha watu wengi kama vile wanabenki, wasambazaji kilimo, wakulima, wafanyakazi wa shamba, madereva wa magari, wahudumu wa vyakula, wasagishaji na waokaji na vilevile hali mbalimbali kama vile hali ya hewa, barabara na uthabiti wa kiuchumi na kisiasa. Ni uchangamano huu ambao hufanya usambazaji wetu kutokuwa na uhakika wa chakula.
- Idadi ya hatua zinazohusika na taratibu zilizo katika kila hatua hutegemea hali mahususi kwa kila jamii na familia. Jedwali ya Mfumo wa Chakula inabainisha hatua na taratibu zinazoweza kuhusika katika mifumo ya chakula cha kutumiwa nyumbani na cha kuuzwa.
- Dhana muhimu ya kufikiria ni uharibifu wa chakula unaotokea kwa sababu ya wanyama na wadudu waharibifu na uharibu katika viwango vya sokoni na nyumbani. Kuvilinda vyakula dhidi ya wadudu, wanyama wenye kudona vyakula, uvunaji na uharibifu unaweza kuongeza kwa kiwango kikubwa kiasi cha chakula kinachopatikana kwa watu kila mwaka utunzaji mbaya na kuoza kwa mazao huharibu mamilioni ya tani za chakula.
Matendo
Kwa kutumia Jedwali ya Mfumo wa Chakula wanafunzi wajiandaye kukamilisha uorodheshaji wa taratibu na utathmini wa kila mojawapo ya hatua zinazohusika katika mfumo wa chakula wanaoutegemea kwa chakula katika jamii yao. Chagua chakula kimoja au zaidi kinacholiwa sana na kutafuta kiini chake, kama mfano wa jinsi mfumo wa chakula cha kienyeji hufanya kazi. Eleza mahali ambapo mfumo wa chakula una udhaifu. Kwa mfano, ikiwa mfumo wa chakula unategemea sana kilimo cha kibiashara, kingetokea nini kama kazi shambani ingekosekana, ikiwa kiangazi kikali kingetokea, ikiwa ghafla barabara zote zinazoelekea jijini zingefungwa, n.k.? Ikiwa mfumo wa chakula wa eneo husika unategemea sana vishamba vya chakula cha nyumbani, eleza kitu ambacho kingetokea iwapo hali (mafuriko, kiangazi) vingeiathiri mimea.
