Lengo 2: Kuelewa maana ya kujitosheleza kwa chakula

Vifaa
Utafiti Maalum wa Nchi
Dhana :Kuwa na uthabiti wa chakula inamaanisha kuwa na uwezo wa wakati wote kukifikia chakula tunachohitaji kwa maisha biabia na yenye afya
Yaliyomo:
- Uhakika wa chakula unaelezwa kama ufikiwaji wa chakula kwa wote kila wakati wa chenye virutubishi vya kutosha na kilicho safi (ubora, wingi na uanuwai) kwa maisha biabia na yenye afya.
- Lazima tujenge hali ambavyo watu wote wanaweza kupata chakula wanachotaka na kuwa na siha nzuri kwa njia nzuri na yenye kudumu.
- Uhakika wa chakula unaathiriwa na maswala mengi, kimsingi: usambazaji wa chakula na kupatikana kwa ajira na huduma nyingine za kimsingi kama vile elimu, vifaa vya afya, usafi,maji safi na makao salama.
- Umaskini, tabaka za kijamii na ukosefu wa elimu ni
viini vya kimsingi vya njaa na ukosefu wa lishe bora na ni vikwazo vikubwa
katika kufanikisha uhakika wa chakula.
Dhana :Uthabiti wa chakula una nguzo tatu muhimu: upatikanaji, ufikiaji na utumiaji wa chakula
Yaliyomo
- Ingawa usambazaji wa chakula ulimwenguni umeongezeka, idadi ya watu ulimwenguni inaendelea kuongezeka kwa kasi sana. Ili kukabiliana na hali hii, uhakika wa chakula kwa wote unaweza tu kupatikana kwa kuzalisha chakula zaidi.
- Hakikisho la uhakika wa chakula haliwezi hata hivyo kupatikana tu kwa kuzalisha chakula zaidi. Ikiwa kwa mfano watu hawawezi kumudu kukinunua chakula kilichopo, ikiwa maakuli yao yanakosa vitamini vya kimsingi na madini ya kimsingi au ikiwa utunzaji wa chakula wakati wa uandalizi (uchambuzi) na ugavi unakifanya kuwa hatari kukila, hawawezi kuwa na uthabiti wa chakula.
Uhakika wa chakula unategemea nguzo tatu au miguu ya kuhimili:
- Chakula lazima kipatikane , kumaanisha kuwa kiasi cha kutosha chenye ubora na salama lazima kizalishwe au kuagizwa kwa viwango vya taifa na maeneo ya kawaida.
- Chakula lazima kiweze kufikiwa , kumaanisha chakula lazima kisambazwe na kuweza kupatikana katika eneo husika, na lazima kila mtu aweze kumudu kukinunua.
- Chakula lazima kitumiwe kwa njia
nzuri iwezekanavyo ili kila mtu awe na siha nzuri (kitoshe kwa wingi, ubora
na uanuwai kulingana na mahitaji na kila mtu).
- Ili kufanikisha uhakika wa chakula kitaifa, nchi lazima iweze kusalisha au kuagiza kutoka nje vyakula inavyovihitaji, na kuweza kukihifadhi, kukisambaza na kuhakikisha usawa katika kukifikia chakula hicho.
- Ili familia kufanikisha uhakika wa chakula, lazima wawe na nyenzo za kuzalisha au kukinunua chakula inachohitaji na lazima wawe na wakati na maarifa ya kuhakikisha kuwa mahitaji ya virutubishi yametimizwa.
Kwa kutegemea uelewa wa uchangamano wa mfumo wa chakula, wanafunzi wanaweza kuchanganua hali maalum, zinazozikabili nchi ili kuamua iwapo maswala ya njaa yaliyopo yanahusiana na upatikanaji, ufikiwaji na utumiaji wa chakula.
- Mafundisho ya thamani yanaweza kufikiwa kwa kuziangazia
nchi ambazo zimefanikiwa kupunguza njaa na kwa kulinganisha hali yao na zile
za nchi ambazo viwango vyao vya lishe vimepungua. Kulingana na hali na
kubainisha mikondo kunaweza kuonyesha sababu zinazochangia matatizo na
suluhisho la njaa ulimwenguni kote. Mifano mahususi ya tafiti katika nchi
zilizo na kupungua na kuongezeka kwa matatizo ya njaa imetolewa katika
(karatasi ya ukweli).
Matendo
- Jadili jinsi hali ni tofauti kabisa kutoka eneo moja hadi jingine, na jinsi mseto wa hali huzua matatizo ya uhakika wa chakula. Kwa kuchanganua nchi zenye viwango vinavyotofautiana vya mabadiliko katika hali yao ya uhakika wa chakula, na kulinganisha hali zilizopo katika kila nchi, mikondo yenye kuonyesha mustakabali wa uhakika wa chakula katika kila nchi unaweza kutambuliwa.
- Mifano halisi ya tafiti ambayo inalingana na hali za zamani na za sasa katika nchi zilizoteuliwa ambapo pametokea mabadiliko ya njaa na uhakika wa chakula yametokea kwa miongo miwili iliyopita. Mifano hii ya tafiti imetolewa kwa jozi, kwa eneo, kulinganisha nchi iliyofanikiwa katika kupambana na njaa na nyingine ambayo imeshindwa kuwalisha watu wake. Wapangie wanafunzi, kila mmoja mmoja au katika makundi mawili moja la tafiti hizo kila moja, au jadili sehemu moja ya tafiti hizo darasani. Kwa msaada wa mwalimu, anapohitajika, wanafunzi watathmini maswala yanyoisababisha hali ya sasa kuhusiana na njaa katika kila nchi. Waeleze wanafunzi kujadili hali zinazohusiana na njaa yaani ya kupatikana,kufikiwa na matumizi ya chakula.
- Kutokana na msingi wa mfumo wa chakula, jadili jinsi
utafiti kama huu ungeafiki katika maeneo yao.
Muhtasari
Azimio letu ni kuwa na hakika kuwa watu wote wana uhakika wa chakula. Kupatikana kwa chakula kunahusisha hatua nyingi. Lazima tuelewe kiini cha chakula chetu ili kufanya maamuzi sahihi kuhusu jinsi ya kumlisha kila mtu ulimwenguni. Somo la 2 lilionyesha uchangamano wa mifumo ya chakula ili kueleza sababu nyingi zinazoweza kuwafanya watu kuwa na njaa, na kuzitalii nguzo za uhakika wa chakula. Baada ya kukamilisha
Somo 2 wanafunzi wanahitaji kuweza kuorodhesha.
- Hatua ya mfumo wa usambazaji wa chakula.
- Kwa kila hatua katika mfumo wa usambazaji chakula, mambo yawezayo kuwatia watu katika hatari ya njaa na uhakika wa chakula.
- Nguzo tatu za uhakika wa chakula
- Mambo ambayo yanasababisha ama kuimarika au kudhoofika zaidi kwa uhakika wa chakula, jinsi inavyoonyesha kwenye mifano ya tafiti zilizofanywa.
Tunaweza kushirikiana kupunguza njaa. Somo 3 litatalii ili kuona mtu anaweza kufanya nini ili kupunguza njaa ulimwenguni.
Kwa kujiunga na Foramu ya KAKN, bonyeza HAPA.
