Sisi, viongozi wa Nchi na Serikali, au wawakilishi wetu, tuliojumuika katika Mkutano Mkuu wa Chakula Ulimwenguni kwa mwaliko wa Shirika la Chakula na Kilimo Ulimwenguni la Umoja wa Mataifa, tunayakinisha tena haki ya kila mtu kukifikia chakula salama na chenye kujenga mwili, sambamba na haki ya kupata chakula cha kutosha na haki ya Kimsingi ya kila mtu kuwa huru kutokana na njaa.
Mjadala: Unakubali kuwa kila mtu ana haki ya kukifikia chakula salama na chenye kujenga mwili na kuwa huru kutokana na njaa? Kwa nini? Inamaanisha nini kuwa na “haki”? tunawezaje kufaulisha hili?
Tunaahidi nia yetu ya kisiasa na kujitolea kwetu sote na kwa nchi zetu katika kufaulisha uthabiti na chakula kwa wote na kwa juhudi inayoendelea ya kuangamiza njaa katika nchi zote, na lengo la mara moja la kupunguza idadi ya watu wenye utapiamlo kufikia nusu ya idadi yao ya sasa kufikia mwaka 2015.
Mjadala: Wakati maendeleo yamepatikana, sasa inaonekana kwamba lengo hili halitafanikishwa. Kutokana na tuliyoyasoma katika somo hili kuhusu njaa, unafikiri ni lini idadi ya watu wenye utapiamlo ulimwenguni wataweza kupunguzwa hadi nusu ya kiwango chao cha sasa? Unafikiri lengo hili linaweza kufanikishwa? Ni nini kinahitaji kufanywa ili lengo hili kufaulishwa?
Tunaiona hali isiyovumilika kwamba zaidi ya watu milioni 800 ulimwenguni kote, na hasa katika nchi zinazoendelea, hawana chakula cha kutosha kukidhi mahitaji yao ya chakula. Hali hii haikubaliki. Hifadhi za chakula zimeongezeka kiasi, lakini vikwazo vya kufikikia chakula na kuendelea kuwepo kwa viwango vidogo vya pato la watu binafsi na nchi ili kununua chakula, kuyugayuga kwa ugavi na mahitaji, na vile vile majanga ya kibinadamu na kimaumbile, huzuia kufanikisha mahitaji ya kimsingi ya chakula. Matatizo ya njaa na uthabiti wa chakula yameenea ulimwenguni kote na huenda yakazidi kuwepo, na hata kuongezeka kabisa katika baadhi ya maeneo, ila pakachukuliwa hatua za haraka, zenye ari na ushirikiano, hasa kwa kuzingatia matarajio ya ongezeko la idadi ya watu ulimwenguni na shirikisho la mali asili.
Mjadala: Kauli hiyo hapo juu inaorodhesha visababishi vitatu vikuu vya ukosefu wa uthabiti wa chakula. Visabavishi hivi ni vipi? (1. Vikwazo vya kukifikia chakula na kuzidi kuwepo pato dogo la watu binafsi na nchi ili kununua chakula; 2. Kuyumbayumba kwa ugawaji na mahitaji; 3. Majanga ya kibinadamu na ya kimaumbile.) Jadili kwa mapana na zaidi kinachomaanishwa na kilamojawapo, visababishi na masuluhisho yake ya kila moja. Je, serikali na watu huweza kufanya nini kuboresha hali hizi?
Tunakariri kuwa hali ya amani na utulivu wa kisiasa, kijamii na kiuchumi ndiyo msingi muhimu ambao utaziwezesha nchi kushughulikia vya kutosha uhakika wa chakula na kuumaliza umaskini. Demokrasia, uendelezaji na utetezi wa haki zote za kibinadamu na haki za kimsingi, ikiwemo haki ya maendeleo, na kushiriki kwa usawa na kabisha kwa wanawake na wanaume ni muhimu katika kufanikisha uthabiti wa chakula kwa wote.
Mjadala: Sehemu hii inapambanua mabadiliko yanayohusiana na haki ya kijamii kwa watu wote, demokrasia, ulinzi wa haki za kibinadamu na haki sawa kwa wanaume na wanawake. Jadili jinsi maswala haya huathiri uthabiti wa chakula katika eneo lako na jinsi mabadiliko ya kijamii na kitamaduni yanaweza kuanzishwa nchini na ulimwenguni kote.
Umaskini ni chanzo kikubwa cha ukosefu wa chakula na maendeleo ya kudumu ni muhimu katika kuondoa umaskini na kuboresha ufikiaji wa chakula. Migogoro, ugaidi, uharibifu wa mazingira pia huchangia pakubwa katika ukosefu wa chakula. Ongezeko la uzalishaji wa chakula, kikiwemo chakula cha msingi, lazima lianzishwe. Hili linafaa kufanyika katika mawanda ya uthabiti unaonufaisha rasilimali, kuondoa kabisa mienendo ya utumiaji na uzalishaji isiyo faida, hasa katika nchi zilizoendelea, na udhibiti wa mapema wa idadi ya watu ulimwenguni. Tunatambua mchango kubwa uthabiti wanawake katika uthabiti wa chakula, hasa katika sehemu za mashambani za nchi zinazoendelea, na haja ya kuhakikisha kwamba kuna usawa baina ya wanaume na wanawake. Uimarishaji wa sehemu za mashambani lazima pia ushughulikiwe ili kuimarisha uimara wa kijamii na kusaidia kuangazia tena tatizo la kiwango kilichopita kiasi cha uhamiaji mijini kutoka mashambani ambalo linazikabili nchi nyingi.
Mjadala: Sehemu hii inalenga maswala makuu ya kilimwengu kama vila njaa vita, ugaidi, ufisadi na uharibifu wa mazingira kama yenye umuhimu katika mapambano dhidi ya njaa. Masuluhisho yanayotolewa ni pamoja na kuongezwa kwa uzajilishaji wa chakula kulinda mali asili na kuondoa pengo kubwa baina ya mataifa na watu tajiri kabisa na maskini kabisa. Haja na usawa baina ya wanaume na wanawake imekaririwa. Sehemu hii inakamilishwa na tatizo kubwa la uhamaji kutoka mashambani kwenda mijini na kupendekeza jukumu la kuyaimarisha maeneo ya mashambani. Jadili maswala haya mapana na nyeti pamoja na wanafunzi. Waulize kufikiria kuhusu jinsi wangeanza kuyashughulikia maswala haya. Kwa kuwa kila mara kuna uhaba wa rasilimali, wangeshughulikia kila kila swala vipi? Wangetumia kigezo gani katika ushughulikiaji huo? Ni suala gani ambalo lina dharura linalohitaji kushulikia kwanza? Lipi rahisi kusuluhisha? Na je, kuhusu ushindani wa raslimali baina ya misaada ya chakula katika hali za dharura na pesa za kazi ya kuimarisha shughuli ya matatizo ya muda mrefu? Yepi yafaa kupewa kipaumbele na kwa nini?
Tunasisitiza umuhimu wa kuchukua hatua sasa ili kutimiza jukumu letu la kufanikisha uthabiti wa chakula kwa vizazi vya sasa na vile vijavyo. Kufanikisha uthabiti wa chakula ni kazi ngumu ambayo jukumu lake la kimsingi ni la serikali zinazohusika. Lazima serikali zijenge hali nzuri na ziwe na sera zinazohakikisha usalama, na vile vile uimara na usawa wa kijamii, kisiasa na kiuchumi na usawa wa kijinsia. Tungependa kueleza masikitiko yetu makubwa kuhusu kuendelea kuwepo kwa njaa ambayo, katika kiwango hiki, inatishia jamii za mataifa na, kwa namna nyingi, kutishia uthabiti wa jamii ya ulimwengu. Katika kiwango cha kimataifa, nchi pia zinahitaji kushirikiana, kushirikiana mashirika y a Umoja wa Mataifa, asasi za kifedha, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, na seckta za umma na zisizo cha umma, kuhusu mipango inayolenga kufanikisha uhakika wa chakula kwa wote.
Chakula kisitumiwe kama kifaa cha shirikisho la kisiasa na kiuchumi. Tunakariri umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa na umoja na vile vile umuhimu wa kijiepusha na hatua zisizo horomo na zisizoambatana na sheria ya kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na ambazo hutishia uthabiti wa chakula.
Tunatambua haja ya kutekeleza sera zenye kusaidia uwekezaji katika uendelezaji wa binadamu, utafiti na miundo msingi ili kufanikisha uhakika wa chakula. Lazima tuhimize kubuniwa kwa kazi na uzalishaji wa mapato, na kuendeleza kufikiwa kuliko sawa kwa raslimali za uzalishaji na za kifedha. Tunakubali kuwa biashara ni sehemu muhimu katika kuleta uthabiti wa chakula Tunakubali kufuatilia sera za biashara ya chakula na sera za biashara kwa jumla ambazo zitawatia moyo wakuzaji na wateja wetu kutumia raslimali zilizopo kwa njia nzuri na yenye manufaa. Tunatambua umuhimu wa uthabiti wa chakula kilicho chenye kunufaisha, uvuvi, misitu na maendeleo ya mashambani katika maeneo yenye uwezo mdogo na hata mkubwa. Tunatambua jukumu muhimu kabisa la wakulima, wavuvi, wanamisitu, watu asili na jamii zao, na watu wengine wote wanaohusika katika sekta ya kilimo, na mashirika yao, kwa misaada ya utafiti na uendelezaji unaofaa, katika kufanikisha uthabiti wa chakula. Sera zetu za maendeleo zenye kunufaisha zitaimarisha kushiriki kabisa kwa watu na kuwapa nguvu, hasa wanawake, usambazaji ulio sawa wa pato, kuweza kupata elimu na huduma za afya, na nafasi mbalimbali kwa vijana. Shughuliko mahususi linafaa kuelekezwa kwa wale wasioweza kuzalisha au kupata chakula cha kutosha kwa maakuli kamilifu, wakiwemo waathiriwa wa vita, migogoro ya kitaifa, majanga ya kimaumbile au mabadiliko ya hali ya hewa. Tunafahamu haja ya kuchukua hatua za dharura kupambana na wanyama na wadudu waharibifu, ukame, na uharibifu wa mali asili kukiwemo usababishaji wa ukame, kuvua kupita kiasi na kuporomoka kwa uhainwai.
Tuna ari ya kuwa juhudi ya kuleta pamoja, na kutumia vizuri rasilimali za utaalamu na fedha zilizotengwa kutumiwa kutoka maeneo yote, ikiwemo kutupiliwa wa mbali madeni ya nchi zinazoendelea, ili kutia nguvu hatua za kitaifa katika kutekeleza sera za uthabiti wa chakula zenye manufaa.
Baada ya kuridhika kwamba uhakika wa chakula wenye sifa anuwai unataka ushirikiano wa kitaifa na juhudi zinazofaa za kimaitaifa ili kuongeza na kutia nguvu harakati za nchi, tunajitolea vifuatavyo:
Tunaahidi utendaji wetu na tunaunga kutekelezwa kwa Mkakati wa Utekelezi wa Mkutano Mkuu wa Chakula Ulimwenguni.
Roma, Novemba 13, 1996