Somo hili limeandaliwa ili lifundishwe kwa dakika 45, pia linaweza kufundishwa kwa undani zaidi au kwa kawaida ili kutosheleza mahitaji ya darasa. Waalimu wanahimizwa kufundisha malengo na maeneo yote yaliyomo. Kwa kila lengo, matendo mbalimbali na viini vya majadiliano yametolewa ili waalimu waweze kuchagua yale yanayowafaa kwa ajili ya wanafunzi wao.
Wanafunzi wanafaa kuelewa kwamba njaa popote pale inawaathiri watu wote, kila mahali, kwamba sote tunahusika katika matatizo ya njaa na ukosefu wa lishe bora, na kwamba kuna hatua mahususi zinazoweza kuchukuliwa na kila mmoja wetu ili kuwa na ulimwengu uliojikomboa kutokana na njaa. Somo linahitaji kuwapa wanafunzi hisia za kusaidia na kujitolea kwa binadamu wenzao na linafaa kuwaonysha kwamba wana jukumu muhimu la kutekeleza katika kupambana na njaa kwa kujipigania wao wenyewe, familia zao, jamii zao na ulimwengu. Mkakati unaotumiwa kupeleka ujumbe huu ni kwa kuzitalii hadithi za mashiyaa ili kuonyesha sababu za mafundisho maadili, imani na udhahiri wa kutoikubali njaa na jinsi sote tunaweza kuwa mashujaa wa kupambana kuimaliza njaa.
Mashujaa Wengi, halisi na wa kubuniwa ni mashujaa kwa sababu ya juhudi zao dhidi ya umaskini na njaa. Kwa kutumia mifano ya hadithi za kiasili, waalimu wanaweza kutumia maelezo yao au yanayopendelewa na wanafunzi ya hadithi za kishujaa, visaasili au watu halisi ili kutanguliza dhana ya mashujaa na kuzijadili sifa za shujaa kuhusiana na kuimaliza njaa.
Lengo 1 linawatambua baadhi ya watu katika historia ambao wamejitahidi kuufanya ulimwengu mahali pazuri zaidi kwetu sote na hivyo kuwahimiza wanafunzi kufikiria kuhusu 'mashujaa' wa kiasili ambao wamezifaidi jamii na nchi zao. Hali hii inaonyesha kuwa sote tuna mchango wa kutoa katika kuimaliza njaa na ukosefu walishe bora na kila mmoja wetu, hata kwa mchango mdogo, anaweza kuwa shujaa kwa mtu mwingine.
Lengo 2 linapendekeza hatua zinazoweza kuchukuliwa na wanafunzi kusaidia kupambana na njaa ukosefu wa lishe bora kwao binafsi, familia na jamii yao. Linawasilisha Azimio la Roma Kuhusu Uhakika wa Chakula Ulimwenguni, lililotiwa sahihi na viongozi wa mataifa wa zaidi ya nchi 180, kama msingi wa mjadala wa kujitolea na mikakati iliyokubaliwa na viongozi wa ulimwengu kuhakikisha uthabiti wa chakula kwa wote. Waalimu wanaweza kuchagua maswala yanayoafiki kati ya mengi yaliyotolewa kuongoza majadiliano darasani kadiri wakati utakavyoruhusu.