Lengo 2:Kutambua hatua mahususi tunazoweza kuchukua ili kusaidia kuimaliza njaa

Vifaa
Karatasi ya ukweli:
Azimio la Roma Kuhusu Uhakika wa Chakula Ulimwenguni
Maelezo:
Kuhusu Siku ya Chakula Duniani
Kulisha Akili, Kupambana na Njaa
Dhana :Tunaweza kuchukua hatua kupunguza njaa na ukosefu wa lishe bora
Yaliyomo:
Serikali za ulimwengu zimejitolea kushirikiana katika tatizo la njaa. Wanafunzi wanahitaji kujua jinsi serikali lilivyojitolea pamoja na mataifa mengine ili kuimaliza njaa.
- Kongamano la kimataifa kuhusu lishe, mnamo mwaka 1992, mataifa 159 na Muungano wa Kiuchumi wa Ulaya ulitoa Azimio Kuhusu Lishe la ulimwengu. Mataifa yote yaliyohusika katika kongamano yalikubaliana kuwa "njaa na ukosefu wa lishe bora' havikubaliki… na ufikiaji wa chakula chenye lishe bora na salama ni haki kwa kila mtu" Mkakati wa kupambana na njaa na kuongeza uhakika wa chakula ulibuniwa.
-
Mkutano Mkuu wa Chakula Ulimwenguni. Mnamo mwaka 1996, zaidi ya mataifa 180 yalishiriki katika mkutano Mkuu wa Chakula Ulimwenguni na kujitolea katika kupunguza idadi ya watu wenye utapia mlo hadi nusu ya kiwango cha sasa kabla ya mwaka 2015. Hati mbili zilibuniwa: Azimio la Roma Kuhusu Uhakika wa Chakula Ulimwenguni, iliyoorodhesha jitihada saba ambazo serikali zilizoshiriki zingefanya ili kuongeza uhakika wa chakula na Mkakati wa Mkutano Mkuu wa Chakula Ulimwengu,
ulioorodhesha malengo mahususi ya kutimiza maazimio yaliyoelezwa kwenye
Azimio. Mataifa yote yaliyohusika yalikubali na kutia sahihi hati hizo, pamoja
na "Tunasisitiza hoja kubwa ya kuchukua hatua sasa hivi ili kutimiza jukumu
letu la kupata uhakika wa chakula kwa vizazi vya sasa na vijavyo".
Tunaweza kujifunza kuhusu njaa kwa njia nyingi. Mashirika na idara zina rasilimali za kutusaidia. Mamia ya mashirika yameanzishwa kushughulikia sehemu mbalimbali za matatizo ya njaa na ukosefu wa lishe bora. Mashirika yanahusisha makundi ya kibinafasi, mashirika ya kiserikali, mashirika ya kimataifa na miungano ya kimaeneo. Yote haya makusudi yao ni pamoja na misaada, utafiti na ushauri. Baadhi ya makundi yamejiingiza katika nchi mahususi, baadhi yao yamejiingiza katika maeneo mahususi kama vile elimu au kilimo.
Matendo:
- Ama mpe kila mwanafunzi nakala ya karatasi ya maelezo Azimio la Roma Kuhusu Uhakika wa Chakula Ulimwenguni, au kwa makundi madogo ya wanafunzi au wasomee wanafunzi kwa sauti - Jadili Kushiriki kwa serikali yao katika Mkutano Mkuu wa chakula mnamo mwaka 1996.
-
Jadili hoja muhimu zilizobainishwa kwenye Azimio, kadiri wakati unavyoruhusu, kwa kutumia maswali ya kujadili yaliyotolewa.
-
Mradi huu - Kulisha Akili, Kupambana na Njaa - umeandaliwa kutoa elimu ili kusaidia kumaliza njaa. Soma au eleza upya kauli inayoeleza malengo na matakwa ya mradi huu. Eleza jinsi wanafunzi wanaweza kunufaika kutokana na kubadilishana habari ambazo wamekusanya kuhusu, njaa, ukosefu wa lishe bora na uhakika wa chakula na madarasa mengine nchini mwao au duniani. Tuna mapendekezo haya kwa Washirika katika Kulisha Akili, Kupambana na Njaa iliyoorodheshwa katika Utangulizi.
-
Siku ya Chakula Ulimwenguni ni shughuli ya kilimwengu ya kila mwaka yenye lengo la kuimarisha ufahamu wa njaa na ukosefu wa lishe bora ulimwenguni na lenye kuwahimiza watu ulimwenguni kote kuchukua hatua dhidi ya njaa. Eleza jinsi darasa la wanafunzi ni mojawapo ya maelfu ya madarasa ulimwenguni kote yanayoshirika katika masomo ya siku ya Chakula Ulimwenguni. Wanafunzi ulimwenguni wanajifunza jinsi wanaweza kushirikiana, ili kuwa sehemu ya kuimaliza njaa. Soma au eleza upya hati Kuhusu siku ya Chakula Ulimwenguni, Oktoba 16, kwa wanafunzi ili waweze kujua baadhi ya juhudi zinazofanywa ulimwenguni kupambana na njaa.
-
Njaa ni tatizo la ulimwengu mzima, lakini sehemu ya suluhisho inahusu hatua nyingi ndogo katika kiwango cha nyanjani. Baadhi ya mifano ya miradi ya ushirika ambayo imeongeza uthabiti wa chakula kwa familia na jamii imeorodheshwa hapa chini. Somo maelezo haya ya miradi kwa wanafunzi na kueleza jinsi miradi mingine sawa na hii inaweza kutekelezwa kiamboni ili kuwafaa watu. Pia eleza jinsi miradi ya aina hii inaweza kufadhiliwa.
- Wanawake wachuuza wa samaki nchini Burkina Faso walinunua masanduku yenye vihami yenye kubebwa kwa baiskeli. Masanduku haya ya barafu hubeba kilo 10 hadi 15 za samaki wabichi, na kuhakikisha kuwa samaki hao waliovuliwa wanauzwa kwa bei ya juu katika soko la kienyeji.
- Wafuga nyuki katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliweza kununua mizinga ya nyuki kwa kiasi kidogo cha pesa za msaada. Mbali na kutoa kilo 15 za asali kila mwaka, nyuki hao wanaeneza chamuua ya miti ya matunda iliyo karibu.
- Nchi ya Nicaragua, wakulima walipata ruzuku ndogo ya kununulia maghala ya chuma ili kuyahifadhi mahindi yaliyovunwa dhidi ya unyevu na wanyama na wadudu waharibifu. Kila bohari linahifadhi kilo 550 za nafaka, kiasi ambacho kinatosha kuwalisha watu kumi kwa mwaka mzima.
- Kwa ufadhili mdogo, wanawake wakulima kutoka Ghana walinunua vifaa vya kutengeza visetiri vya urefu wamita 501 mraba ili kuhifadhi miche yao ya ndizi kutokana na jua kali barani Afrika.
- Kundi la wakulima wa Senegalo walishirikiana kununua pampu inayofanya kazi kwa shirika la kukanyaga, yenye uwezo wa kunyunyizia hadi eneo mraba la miti 2500 la mboga kwa kutumia maji kutoka kwenye kusoma kidogo kilichochimbwa kwa mikono.
- Chama Cha Shirika chaa wakulima kiliekeza katika
mbegu za ubora wa juu na kupanda ekari 20 za kabeji, vitunguu, mboga zingine
na viazi pamoja na mbegu za mimea yenye kuzalisha chakula cha wanyama ili
kulisha wanyama wao.
- Tunaweza kupata habari kuhusu njaa katika jamii zetu na katika ulimwengu kutokana na asili nyingi. Tunaweza kuandika barua, kuwatembelea watu au kupiga simu maofisini na kwenye maktaba. (Inapowezekana, kutafuta kwenye mtandao.)
- Wasiliana na au waambie wanafunzi kuwasiliana na mashirika ya kimataifa yaliyo Washirika Katika Kulisha Akili, Kupambana na Njaa. Baadhi ya Mashirika haya yana wawakilishi wa nchi au maafisa wa miradi nyanjani ambao wanaweza kukutana nao na kuwaalika shuleni kuzizungumzia kazi zao. Yaombe mashirika hayo kutuma habari kuhusu miradi yao au kuhusu shughuli zao za kumaliza njaa zinazoweza kulishirikisha darasa.
- Liambie darasa kuwasiliana na wengine wanaohusika na mashirika ya njaa, viongozi wa nyanjani, wa kitaifa, wa jimbo au wa kimataifa na kuwauliza kinachofanywa kuhusiana na kila mojawapo ya nguzo za misaada wa uhakika wa chakula (kama ilivyojadiliwa katika masomo yaliyotangulia) Aidha, waongoze wanafunzi kutafuta au kuomba habari inayoonyesha kiasi cha njaa katika maeneo yao.
- Wasiliana na mamlaka ya umma mitaani na kuyaalika darasani kuzungumzia kuhusu hatua zinazochukuliwa nyumbani ili kuzuia njaa na ukosefu wa lishe bora. Wanafunzi wawahoji maafisa kadha wa umma kuhusu miradi au shughuli za njaa nyanjani kila mwanafunzi au kundi la wanafunzi linaweza basi kuandika ripoti fupi kwa muhtasari na kuiwasilisha darasani.
- Kusanya habari (au waeleze wanafunzi kukusanye habari) kuhusu hatua zinazochukuliwa katika eneo husika kuhakikisha kuwa kuna usambazaji thabiti wa chakula. Waalike wanachama wa mfumo wa chakula na elimu darasani kujadili jinsi ukakika wa chakula unatunzwa katika eneo lenu. Jaribu kujadili kiasi cha chakula kilichohifadhiwa katika eneo lenu kwa ajili ya dharura. Je, watu wanajua la kufanya itokeapo tatizo la chakula? Kwa kuutegemea msingi wa habari kuhusu matatizo ya njaa nyanjani kutoka Somo 1, waulize wanafunzi jinsi matatizo ya nyanjani kuhusu njaa yanavyoweza kupunguzwa.
- Jadili umuhimu wa elimu katika kupambana na njaa. Kiasi kikubwa cha njaa kinahusiana na umaskini unaotokana na ukosefu wa elimu. Wanafunzi wahimizwe kuwa shuleni na kujifunza mengi iwezekanavyo kuhusu kilimo cha lishe pamoja na maarifa ya kimsingi.
- Jadili manufaa ya taaluma ya huduma za jamii na kupambana na njaa na jinsi wanafunzi wanaweza kujifunza kusaidia katika eneo hili. Waalike wakala wa nyanjani wa afya na wengineo darasani kuzungumzia jinsi watu wengi wanahitajika katika maeneo yanayohusiana na kupambana na njaa.
- Waambie wanafunzi kutoa maoni yao kuhusu hatua ambazo
wao, na wengine, wanaweza kuchukua katika jamii yao ulimwenguni ili kusaidia
kutatua matatizo ya njaa na ukosefu wa lishe bora. Orodhesha hatua hizo na
kutambua ni nani anayeweze kuzitekeleza. Orodha ya baadhi ya hatua
zinazochukuliwa ulimwenguni imetolewa hapo chini. Onyesha mfano mmoja au
miwili kati ya orodha iliyotolewa na wanafunzi au kutoka kwenye orodha
iliyotolewa, na kuchunguza jinsi hatua hizi zinaweza kutekelezwa na jinsi
ambavyo hatua hizi zingesaidia kupambana na njaa nyanjani au ulimwenguni.
Mifano ya vitendo:
Kusaidia kuongeza utoaji wa chakula kwa kuboresha chakula na aina tofauti ya vyakula vinavyopatikana:
- tumia bustani za jumuiya na za shuleni ili kupanga chakula
- fuga kuku na wanyama wadogo nyumbani kwa ajili ya kula au kwa biashara
- jaribu kugundua tena vyakula vilivyosahulika na vinavyostawisha katika eneo lako
- kuza mazao yaliyo bora kwa ajili ya chakula na biashara
- kuza mazao yanayositahimili udongo na maji ya eneo husika
- tumia vitendea kazi vinavyopatikana kwa ajili ya kilimo katika eneo hilo
- tafuta uwiano mzuri kati ya mazao ya biashara na chakula
- jiingize katika shughuli za shirika katika kukuza na kuuza mazao
- unga mkono wakulima wazawa; kwa kununua mazao yao
- anzisha vituo au maeneo ya kuhifadhia ya chakula cha
mgao
Saidia kuweka chakula salama kwa ajili ya matumizi ya baadaye:
- weka chakula sehemu safi na salama
- weka sehemu ya maandalizi ya chakula na vitendea kazi katia hali ya usafi
- weka chakula cha ziada katika maeneo makavu, mbali na
wadudu na wanyama
Wasaidie watu wote kukidhi mahitaji yao ya chakula na virutubishi:
- zifahamu hoja zako za chakula na virutubishi
- zifahamu haja mbalimbali za watu mbalimbali(hatua za maisha)
- tafuta vyakula vipatikanavyo vyenye kuleta siha nzuri
- jitolee kuhudumia maswala ya njaa
- jitolee kufanya kazi katika vituo vya usambazaji chakula.
- jenga vituo vya vyakula au maghala ya chakula ili kugawanya chakula cha ziada
- shirikiana na viwanda vya chakula ili kukisambaza tena chakula cha ziada
- waalike wakulima wa vyakula vya kuuza na wakuzaji ili
wawe sehemu ya suluhisho la matatizo ya njaa katika jamii.
Jifunze kuhusu vyakula, lishe na njaa na kuyatoa maarifa na mawazo kwa wengine.
- jifunze kuhusu mfumo wa chakula katika eneo lako
- fahamu ni nani katika jamii yako wanajitahidi kupambana na njaa, wasikilize, na kubadilishana mawazo nao
- fahamu ni nani katika jamii wana maarifa kuhusu afya na kubadilisha mawazo nao
- chukua habari nyumbani kwa familia na majirani
- badilishana ripoti na miradi ya shule katika maeneo ya kijamii
- badilishana mawazo na viongozi katika jamii na taifa
- wahimize viongozi wa jamii na watoa huduma (madaktari
/ wauguzi / wafanyakazi wa hospitali / waktubi) kushiriki katika miradi ya
shule inayohusu maswala ya njaa na lishe.
Muhtasari
Katika masomo matatu ya mtaala huu, ambayo awali yaliandaliwa Siku ya chakula Ulimwenguni, Oktoba 26, 2001 tuyaangazia matatizo ya njaa ulimwenguni. Lengo la Siku ya Chakula Ulimwenguni ni kuimaliza njaa haraka iwezekanavyo katika kikwi kipya. Mamilioni kati yetu hadi leo bado hawana chakula cha kutosha kwa kila siku. Lazima sote tujaribu kuelewa kwa nini kuna hali hii. Vijana wana ubunifu na nguvu za kuyakabili matatizo makubwa kama vile njaa. Wakati ambapo sote tutakuwa na mtizamo wa ulimwengu usio na njaa, ushupavu ni kwamba tunaweza kurekebisha mambo, ufahamu wa hatua za kuchukua na nia ya kuchukua hatua, tunaweza kusuluhisha daro kubwa la kuwalisha watu wote wa ulimwengu. Nao vijana, wetu waliorithi tatizo la ulimwengu, watakuwa msingi wa kupata suluhisho.
Kwa kujiunga na Foramu ya KAKN, bonyeza HAPA.
